Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Pratap Ghose akizungumza wakati wa kuzindua ofa mpya ya Kula Tano kwa wateja wa Zantel, ambayo inawazawadia wateja wao dakika za bure kwa kupokea simu zao.
Meneja wa Zantel, Deus Mtena akizungumza wakati wa uzinduzi wa ofa ya Kula Tano katika ofisi za Zantel. Anayetazama kushoto ni Meneja wa Huduma, Ashish Singh.
Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Pratap Ghose akigawa vipeperushi vya ofa ya Kula Tano baada ya kuizindua katika ofisi za Zantel.
Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Pratap Ghose akigawa vipeperushi vya ofa ya Kula Tano baada ya kuizindua katika ofisi za Zantel.
Dar es Salaam, 22/9/2015: Kampuni ya simu ya Zantel leo imezindua ofa mpya ya
kuwazawadia wateja wake dakika za ziada kila mara wanapopokea simu kutoka
mitandao yote katika simu zao za mikononi.
Ofa hiyo inampa kila
mteja wa Zantel dakika moja ya bure kila akipokea simu ya zaidi ya dakika nne
ya ndani ya mtandao na pia atapata dakika nne za bure akipokea simu kutoka
mitandao mingine kwa zaidi ya dakika mbili.
Akizungumza wakati wa
uzinduzi wa ofa hiyo, Mkurugenzi wa Masoko wa Zantel, Progress Chissenga
alisema ofa hii imezinduliwa maalumu ili kuwapa wateja wa Zantel thamani ya
fedha zao pamoja na fursa ya kufurahia zaidi huduma za mtandao huo.
‘Leo tunazindua ofa
mpya na ya kipekee kabisa katika soko kwa wateja wetu wa Zantel, ambayo kila
mtumiaji wa mtandao wetu atazawadiwa dakika za bure kwa kupokea tu simu yake’
alisema Chissenga.
Akielezea zaidi
kuhusu ofa hiyo, Chissenga alisema hakuna mtandao uliowahi kuwazawadia wateja
wake kwa kupokea tu simu, na hivyo ofa hii ni ya kwanza nchini ambayo itawapa
wateja nafasi ya kufurahia dakika za bure ambazo wanazoweza kupiga kwenda
mitandao yote.
‘Zantel inawajali
wateja wake na itaendelea kuhakikisha inakuwa zaidi ya mtandao wa simu kwa
kuwapa wateja wake fursa ya kuwasiliana zaidi iwe na ndugu zao au kibiashara’
alisema Bi Chissenga.
Mwisho Bi Chissenga
alisema ofa hii itakuwa mkombozi kwa wateja wasio na kipato lakini wanatumia
huduma ya Zantel kwani wataweza kujipatia dakika za bure kila mara wanapopokea
simu katika simu zao za mikononi na hivyo kuwawezesha kuendelea kuwasiliana
na ndugu na jamaa zao.
No comments:
Post a Comment