Habari za Punde

Wafanyakazi wizara ya Afya wawaaga Waziri, Naibu Waziri leo

 Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa Wizara hiyo (hawapo pichani) waliofika katika sherehe za kuagwa kwao zilizofanyika Wizara ya Afya Mjini Zanzibar. Kushoto Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman.
 Baadhi ya Mafisa wa Wizara ya Afya Zanzibar wakisikiliza nasaha kutoka kwa Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo (hayupo pichani) katika sherehe za kuaaga zilizofanyika Wizara ya Afya.

 Waziri wa Afya Zanzibar Rashid Seif Suleiman akitoa nasaha zake na kuwashkuru watendaji wake kwa mashirikiano yao katika sherehe za kuagwa kwao zilizofanyika Wizara ya Afya, (kushoto) Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Mohammed Jidawi na (kulia) Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo. 
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Mohammed (kushoto) akimkabidhi zawadi Waziri wa Afya Zanzibar Rashid Seif Suleiman katika sherehe za kuagwa kwao zilizofanyika Wizara ya Afya Mjini Zanzibar. 
Dua baada ya Sherehe. 
Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.