Habari za Punde

Mawakala wa vyama vya siasa wapatiwa mafunzo ya kuchaguzi Wilaya ya Magharibi

DSC03948
Msimamizi wa Uchaguzi wilaya ya Magharib ” A”  Mwalim Khamis Mussa akitoa ufafanuzi wa masuala ya kiuchaguzi katika semina ya mawakala wa vyama vya siasa wa vituo vya Uchaguzi  vya wilaya ya magharib A na B, semina hiyo ilfanyika tarehe 22/10/2015 skuli ya Mwanakwerekwe “C” Mjini Zanzibar.
Aidha, Mwalim Khamis aliwataka mawakala hao kufuata sheria na kanuni za uchaguzi pamoja na maelekezo ya Tume ya Uchaguzi na badala yake waache maneno ya wanasiasa ili kuwa na Uchaguzi huru na wa amani
DSC03966
Msaidizi Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mwera Ndg. Juma Moh’d akitoa mafunzo kwa mawakala wa vyama vya siasa ambao watasimamia mwenendo wa Uchaguzi katika vituo vya Kupigia Kura vya wilaya ya Magharib A na B, mafunzo hayo yalitolewa skuli ya Mwanakwerekwe “C” tarehe 22/10/2015.
DSC03946
Mawakala kutoka vyama vya siasa ambavyo vitashiriki katika Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wakiwa katika mafunzo ya kiuchaguzi ambayo yalitolewa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Wilaya ya Magharib A na B Tarehe 22/10/2015 skuli ya mwanakwerekwe “C” Zanzibar.
Mafunzo hayo ya mawakala wa vyama vya Siasa yalifanyika kwa wilaya zote Unguja na Pemba ili kuhakiksha Uchaguzi unakuwa huru na haki.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.