Habari za Punde

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Azungumza na Waandishi wa Habari Zanzibar.

 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Mhe Vuai Ali Vuai akizungumza na waandishi wa habari kulaani kitendo cha CUF,kujitangazia ushindi wakati wa mazungum na waandishi wa habari wa vyombo mbaklimbali jana kukiuka taratibu za Sheria za Tume ya Uchaguzi Zanzibar ya kutangaza matokeo, mkutano huo na waandishi wa habari umefanyika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM kisiwandui Zanzibar jana jioni. 
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Mhe Vuai Ali Vuai akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali Zanzibar kutokana na Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar uliofanyika jumapili.
Viongozi CCM wakiwa katika ukumbi wa mkutano Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar, wakati wa mkutano na waandishi wa habari wa Vyombo mbalimbali Wanaoripoti habari za Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar.
 Waandishi wa habari wakifuatilia mazungumza na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Mhe Vuai Ali Vuai, katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandu Zanzibar na kulaani kitendo cha Mgombea wa CUF kujitangaza ameshinda Uchaguzi wa Zanzibar.
 Waangalizi wa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar kutoa Nje wakifuatilia mkutano na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Mhe Vuai Ali Vuai, uliofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.
 Mkujumbe wa Kamati Kuu ya CCM Mhe Shamis Vuai Nahodha akizungumza na waandishi wa habari na kutoa ufafaniuzi wa Sheria za Uchaguzi wakati wa mkutano na waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali Zanzibar uliofanyika Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.

 

1 comment:

  1. nyie basi tena mushachokwa munalazimisha tu, hamufahamu nyinyi?

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.