Habari za Punde

Tatizo la vifo vya mama na mtoto wakati wa uzazi latafutiwa ufumbuzi wa kudumu


Na Masanja Mabula –Pemba .

WIZARA ya afya visiwani Zanzibar imesema kuwa tatizo la vifo vya Mama na Mtoto vinavyotokana na uzazi bado linaendelea kutafutiwa ufumbuzi huku ikizitaka taasisi zinazohusika na utoaji wa elimu ya uzazi kuongeza juhudi kuielimisha jamii jinsi ya kukabiliana na tatizo hilo .

Katibu Mkuu wa Wizara ya afya Zanzibar Dk Mohammed Saleh Jidawi ameyasema hayo wakati akizindua mradi wa ushirikiano kati ya serikali wizara ya afya na UMATI wa uimarishaji uhusiano kati ya jamii katika kutoa huduma shirikishi ya afya ya uzazi ,mama na mtoto na VVU   utakaoendeshwa na Chama Cha Malezi Bora Tanzania  (UMATI)  na kufadhiliwa na Japan Trust Fund .

Amesema kuwa vifo vya mama na mtoto ni moja ya changamoto zinazohitaji mikakati madhubuti kupitia serikali , Wizara ya afya pamoja na wadau wengine wa huduma ya uzazi kwani zinazidi kupoteza maisha ya mama na watoto .

  Jidawi amesema kwamba asilimia 28 ya vifo vya watoto hutokea katika kipindi cha siku ishirini na nane (28) baada ya kujifungua na kufahamisha kwamba mradi huo ndiyo mwarubaini wa vifo hivo kwani jamii itakuwa na uelewa wa kutosha juu ya huduma za uzazi .

“Wizara bado inasikitishwa na vifo vya mama na mtoto ambavyo hutokea baada ya kujifungua  lakini kuzinduliwa kwa mradi huu kumenipa matumaini ya kulimaliza tatizo hili ”alieleza Dk Jidawi .

Aidha Katibu Jidawi  amesema katika kuunga mkono mradi huo ,wizara ya afya itachangia rasilimali watu ikiwa ni pamoja na vifaa , wataalam , usafiri na majengo ambayo yatatumika katika kutoa huduma kwa jamii .

Naye balozi wa Japan Nchini Tanzania Masaharu Yoshida amesema kuwa Japan itaendelea  kuisaidia miradi ya maendeleo kwa Tanzania hukuakipongeza UMATI kwa uwamuzi wa kuanzishamradi huo ambao umelenga kuboresha afya za wananchi .

Balozi Yoshida amesisitiza  haja kwa wananchi wa Zanzibar kushirikiana na watendaji wa UMATI pamona na Wizara ya Afya katika kufanikisha malengo ya mradi huo .

“Natambua kwamba afya bora ni mtaji , hivyo ni vyema wananchi wa Pemba hususani Mkoa wa Kaskazini Pemba kutoa ushirikiano ili kufanikisha utekelezaji wa mradi  huu ”alisisitiza Yoshida .

Mapema akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba  ,Mkuu wa Wilaya ya Wete , Hassa Khatib Hassaan ameziagiza Halmashauri yaWilaya ya Micheweni na Wete pamoja na Baraza la Mji Wete kusimamia utekelezaji wa mradi huo .

Amesema kuwa kwa mradi huo utekelezwa katika maeneo  yaoni budi kuhakikisha kwamba wanawaelimisha wananchi ili waweze kutoa msaada ya ushiriki mzuri wakati wote wa utekelezaji wamradi huo .

“Serikali za Mitaa hili ni jukumu lenu hakikisheni kwamba wananchi wa shehia zilizochaguliwa wanapata elimu na wanashiriki katika utekelezaji wa mradi huu ”alisisitiza Hassan Khatib Hassan ..

Mradi huo wa miaka miwili utatekelezwa katika shehia kumi na mbili (12) za Mkoa wa Kaskazini Pemba na umekuja kutokana na shehia hizo kubainika kuwa nyuma katika maswala ya huduma za mama ana mtoto .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.