Habari za Punde

Kesho ni siku ya mapumziko

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 4(m) cha sheria Nam. 7 ya mwaka 1984 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Dkt. Ali Mohamed Shein ametangaza kwamba kesho Alhamis tarehe 5 Novemba, 2015 itakuwa siku ya mapumziko ili kuwawezesha wananchi kushiriki katika sherehe za kuhitimisha Uongozi wa Awamu ya nne ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuanza kwa  Awamu ya tano ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Uongozi wa Dkt John Pombe Joseph Magufuli .   

MWISHO

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.