Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na waandishi wa Habari katika ofisi za CUF Mtendeni kuhusiana na maendeleo ya “mkwamo” wa kisiasa Zanzibar. (Picha na Salmin Said, OMKR)
Na: Hassan Hamad (OMKR)
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amesema jitihada za kuutafutia ufumbuzi mkwamo wa kisiasa Zanzibar uliotokana na tamko la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Bw. Jecha Salim Jecha baada ya kutangaza kufuta uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba 2015, zinaendelea vizuri.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za CUF Mtendeni mjini Zanzibar, Maalim Seif ambaye pia ni mgombea Urais kupitia Chama hicho amesema ana matumaini kuwa suala hilo litapatiwa ufumbuzi wa haki unaoheshimu maamuzi ya wapiga wa Zanzibar waliyoyafanya tarehe 25 mwezi uliopita.
Amefahamisha kuwa jitihada hizo zimekuwa zikifanywa na taasisi mbali mbali za ndani na nje ya nchi zikiwemo Umoja wa Mataifa pamoja na nchi kadhaa ambazo ni marafiki wa Tanzania zikiwemo zilizoleta waangalizi wa kimataifa katika uchaguzi huo.
Amesema jitihada pia zimekuwa zikifanywa na viongozi wakuu wastaafu, viongozi wa dini na Msajili wa vyama vya siasa Tanzania Jaji Francis Mutungi.
Ameeleza kuwa Chama Cha Wananchi CUF kimetiwa moyo na imani kutokana na jitihada hizo, na kwamba ufumbuzi wa haki wa suala hilo utapatikana katika kipindi kifupi kijacho.
Maalim Seif ametumia fursa hiyo kuwataka Wazanzibari waendelee kubaki watulivu na kuitunza amani ya nchi, na kuwaaachia viongozi wao kulifanyia kazi suala hilo kwa kushirikiana na watu mashuhuri pamoja na Taasisi za kitaifa na kimataifa.
Amewaomba wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama kufanya juhudi kuhakikisha Zanzibar inabaki katika hali ya amani na utulivu, na kutokubali kutumiwa na wanasiasa kufanikisha mbinu chafu ambazo zinaleta taharuki na hofu miongoni mwa raia.
Maalim Seif amewahakikishia viongozi na wanachama wa CCM na Wazanzibari wote kwamba iwapo atatangazwa mshindi wa uchaguzi huo hakutokuwa na ulipizaji wa kisasi, na kwamba atafanya kazi kwa ushirikiano chini ya muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa maslahi ya Zanzibar.
Maalim ukikubali uchaguzi urejewe ndo umepigwa bao, mana mimi naamini wameshindwa kufanya mambo yao kwasababu hawakupata msaada kutoka bara, maana huko bara nako CCM walikuwa mavi kitambaani sasa ukirudiwa watakuwa washatuliza akili zao watakupiga mabao ya mkono tena mingi
ReplyDeleteKitendo cha kujitangazia ushindi wa urais kabla ya ZEC kukamilisha uhakiki wa kura ni kosa la jinai ambalo mtendaji ahukumiwe na adhabu yake ni miaka 5 jela au faini mil 5 au vyote viwili.
ReplyDeleteSasa si wakimfikishe kwenye vyombo vya sheria na kumchukulia hatua, kwanini wanambembeleza?
ReplyDeleteKuendelea kumuacha huru, ndiko kunakopelekea baadhi ya watu waone kuna jambo linafichwa.
Migogogro ya namna hii, inatuumiza sana kiuchumi, lkn. ni wachache tu baina yetu wanoaliona hilo, walio wengi wanadhani serikali ni DUDU KUBWA ambalo haliwezi kushindwa kuhudumia wananchi wake, jambo ambalo sio kweli.
Leo hii, badala ya kushughulikia shida za wananchi kama vile matibabu na maji nk. sisi tunatatua migogoro ya kisiasa isiyokwisha.
Wenzetu Bara wanatusifia UJINGA kwamba siasa za Z'bar ni ngumu huku wao wanafanya maendeleo yao.
Ukishuka Bandarini Dar utadhani upo ulaya wakati kwetu Visiwa vimejinamia kama vile wenyewe wamekufa, ukiumwa kidogo tu lazma upelekwe Bara sijui mpka lini?
Mie nadhani mambo haya yafikie mwisho..hata wenzetu wanatusaidia tu lkn wa-llwahi wanatudharau!
Mimi nashangaa wale wanaosema kuwa chama flani kujitangazia kushinda uchaguzi ni kosa la jinai! Nchi ambazo ni huru duniani ndivyo ilivyo na chama tawala kinapokea taarifa hizo toka mawakala zao na hukubali kuwa wameshindwa katika upigaji kura kwa nini Zanzibar au Tanzania iwe kosa la jinai? Alieweka sheria hio aliweka kuwagandamiza wapinzani wake kwa kuwaziba mdomo hakuna chengine!
ReplyDelete