Habari za Punde

Jopo la Umoja wa Mataifa Linaloongozwa na Jakaya Mrisho Kikwete Lakamilisha kazi Yake New York, Marekani

Jopo la Watu Mashuhuri la Umoja wa Mataifa la Kupendekeza Namna Bora ya Dunia Kukabiliana na Majanga ya Afya limekamilisha kazi yake wiki iliyopita jijini New York.
 
Jopo hilo linaloongozwa na Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete lilikabidhiwa jukumu hilo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki moon tarehe 2 Aprili, 2015 na kupewa muda wa kuanzia Mei hadi Desemba 2015 kukamilisha kazi yake.

Jopo limefanya mikutano minne na kukutana na wadau mbalimbali wa afya zikiwemo taasisi za Umoja wa Mataifa, wadau wa maendeleo, wataalam mbalimbali na kupokea maoni na uzoefu kutoka kwa nchi zilizoathirika na ugonjwa wa Ebola.

Watu mashuhuri wanaounda Jopo hilo ni Mheshimiwa Michelin Calm-Roy aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Uswisi; Mheshimiwa Marty Natelagawa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Indonesia; Mheshimiwa Joy Phumaphi, aliyekuwa Waziri wa Afya wa Botswana na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Mheshimiwa Celso Amorim aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Brazil na Rajiv Shah aliyekuwa Mkuu wa Shirika la Misaada na Maendeleo la Marekani (USAID).

Jopo hilo linatarajia kuwasilisha ripoti yake kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mwezi January, 2016 na baadae kuwasilishwa kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. 
Mwenyekiti wa Jopo, Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete akiendesha Mkutano wa Jopo.
Wajumbe wa Jopo katika Picha ya Pamoja na Wajumbe wa Sekretariati ya Jopo.
Wajumbe wa Jopo la Watu Mashuhuri la Umoja wa Mataifa la Kushauri Dunia Namna Bora ya Kukabiliana na Majanga

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.