Habari za Punde

Waraghbishi wa kijiji cha Nyandekwa na Harakati za Kumkomboa Mwanamke

Baadhi ya waraghabishi wa kijiji cha Nyandekwa Wilayani Kahama wakiongea na waandishi wa habari waliofika kijijini hapo kwa ajili ya kujionea matokeo mbali mbali baada ya waraghabishi kuwasaidia wananchi hao kuchukua hatua katika kila jambo kwa maendeleo ya kijiji chao
Pichani nikihoji maswali kwa Dada Miriam Stefano  (Aliyejishika tama ) ambaye amekuwa mchango mkubwa kwa kutoa elimu ya uzazi na mabadilko ya mwili kwa vijana wa kike katika baadhi ya shule za sekondari na msingi katika kijiji hicho 

Picha ya pamoja nikiwa na waraghabishi wa kijiji cha Nyandekwa  Wilayani na waandishi wa habari tuliopata bahati ya kutembelea kijiji hicho na kujifunza namna gani wameweza kuwa chachu ya maendeleo katika kijiji hicho

Na Krantz Mwantepele ,KAHAMA
Mkutano mkuu wa Kijiji cha Nyandekwa wilayani Kahama mkoani Shinyanga uliofanyika mwishoni wa mwezi wa tisa umeazimia kuwashikinikiza wazazi wa kijiji hicho kuwapeleka watoto wao shule  Azimio hilo Pia limeelekezwa  kwa vijana wanaokaa vijiweni kuwataka kushirki katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na sio kukaa vijiweni pia kushiriki katika mikutano mbali mbali ya kijiji kujua maendeleo ya kijiji  Iikihusisha mapato na matumizi.

Mkutano huo umepitisha maazimio matano  yanayolenga kurejesha nidhamu Na heshima kijijini Nyandekwa hatua hiyo imefikiwa Kutokana Na wananchi wa kijiji hiki kutoona umuhimu wao kuchukua hatua za kujikwamua kiuchumi na pia Kuwa na ujasiri wa kuhoji mapato na matumizi kwa ajili ya kijiji chao .

Hali hiyo inatokana na juhudi za dhati bila kukata tamaa zilizofanywa waraghabishi  na watetezi wa haki za binadamu wa kijiji hicho akiwemo Miriam Stefano, Boniface Izengo , Matilda Peter ,Na Mwenyekiti Wa kitongoji cha  Busolwa Bi Ana Alphonce kuwapa ujasiri  na elimu ya uraia wananchi wenzao ili wawe chachu ya maendeleo.


Kwa mujibu wa bi Anna Alphonce ambaye pia ni mwenyekiti wa kitongoji cha   Busolwe aliweza kuongea na mtandao wa Mwanaharakati Mzalendo Blog alisema kupitia mikutano mbalimbali ya kijiji aliweza kutoa hamasa kwa wanawake na wanaume wa kijiji hicho kushiriki katika uchaguzi mkuu uliopita katika kusikiliza sera za viongozi na mwishowe kushiriki kupiga kura.Na kwa muda mfupi aliweza kufanikisha wanawake wengi kushiriki katika maamuzi ya kijiji pia kuwa na ujasiri wa kuhoji katika mikutano ya kijiji.

Wengi wa wanakijji ambao wamekuwa waraghabishi katika kijiji hiki waliweza kupata mafunzo haya ya uraghabishi ambapo waliweza kujua baadhi ya haki zao na kuwa na uajasiri wa kuhoji mapato na matumizi ya kijiji hicho ambapo mwanzoni walikuwa hawapati fursa hiyo kwa wakati .Waraghabishi hawa wamekuwa chachu ya maendeleo ya kijiji cha Nyandekwa katika sekta za kiuchumi ,kisiasa na kijamii kwa kuwaelimisha wanakijiji wenzao haki na wajibu wao kwa nafasi kubwa .

“Viongozi wa kijiji hiki hawakuweza kutupa mrejesho wa kila jambo linalofanyika kwa kijiji hcetu hasa katika mikutano ya kijiji na sisi tulipoanza kuhoji tulikosa ushirikiano kwao lakini mwishowe wananchi wengi waliona umuhimu wa kushirikishwa”   alinukuliwa  bw. Boniface Izengo mmoja wa waraghabishi wa kijiji hiki alipokuwa akiongea na mwandishi wa habari hii.

Katika hatua nyingine mmoja wa waraghabishi wa kijiji hiki Bi Matilda Peter amekuwa ni mmoja wa vijana wanaotoa elimu ya uzazi wa mpango kwa makundi rika ambapo hukutana na vijana hasa wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari na kuwajuza kuhusu mabadiliko ya mwili yao na pia kuwashauri jinsi ya kuepuka maambukizi magonjwa ya ngono na mimba zisizotarajiwa.
 Maazimio yaliyopitishwa kuwa ni vijana wanaokaa au kusimama ovyo barabarani na maeneo mengine bila shughuli maalum kuwajibishwa na pia kuweza kuwawezesha kuwashirikisha katika shughuli za kijiji hicho ikiwemo kushiriki katika shughuli mbalimbali za uzalishaji kijijini hapo.
Pia mkutano wa kijiji hiki uliazimia kuwa mapato na matumizi kuweza kujadiliwa kwa uwazi na pia kubandikwa katika mbao za matangazo hapo kijijini kuwezesha wananchi hao kuweza kusoma na kuelewa kila kinachoendelea kijijini kwao katika swala la maendeleo ya uchumi .
.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.