Habari za Punde

Katibu Mkuu Mpya wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Ajitambulisha kwa Watumishi – Awataka Kufanya Kazi kwea Bidii

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya 

Nchi, Mbarak Abdulwakil ambaye sasa ni Katibu Mkuu, Ofisi 

ya Makamu wa Rais, akiwaaga watumishi wa Wizara ya 

Mambo ya Ndani ya Nchi (hawapo pichani) katika mkutano 

uliofanyika katika Makao Makuu ya Wizara hiyo. Katikati ni 

Katibu Mkuu mpya wa Wzara hiyo, Meja Jenerali Projest 

Rwegasira na kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Balozi Hassan 

Simba Yahaya.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, 

Balozi Hassan Simba Yahaya, akijitambulish kwa Watumishi 

wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, katika mkutano 

uliofanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo.  Katikati ni Katibu 

Mkuu wa Wizara, Meja Jenerali Projest Rwegasira na 

kushoto ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak 

Abdulwakil, ambaye sasa ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu 

wa Rais.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, akizungumza na Watumishi wa Wizara hiyo, katika mkutano wa kujitambulisha uliofanyika Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani Nchi. Meja Jenerali Rwegasira aliteuliwa hivi karibuni kuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.
 Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil ambaye sasa ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, akimkabidhi Katibu Mkuu mpya, Meja Jenerali Projest Rwegasira, moja ya Nyaraka za Ofisi za Wizara hiyo kama ishara ya kumkabidhi ofisi.
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakiwa katika mkutano wa kumuaga aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil, ambaye sasa ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, na kuwakaribisha Katibu Mkuu mpya, Meja Jenerali Projest Rwegasira na Naibu Katibu Mkuu, Balozi Hassan Simba Yahaya.  Hafla hii ilifanyika katika Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali  – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.