Habari za Punde

Yanga Yafanikiwa Kuingia Nusu Fainali Kombe la Mapinduzi kwa Kuifunga Mtibwa 2--1


Wasemaji wa ya Yanga, Simba na Azam wakiwa katika uwanja wa Amaan Zanzibar akifuatilia mchezo wa Kombe la Mapinduzi kati ya Timu ya Yanga na Mtibwa lililofanyika jana usiku na Timu ya Yanga kuibuka mshinda wa Pambano hilo kwa kuitwanga timu ya Mtibwa kwa mabao 2--1 na kufanikiwa kuongoza kundi hilo kwa kufikisha point 7 na Timu ya Mtibwa kuchukua nafasi ya Pili kwa kufikisha point 4, na timu za Mafunzo na Azam kuwaaga mashindano hayo katika hatua ya mwazo ya makundi. 
Benchi la Ufundi la Timu ya Yanga wakifuatilia mchezo wao wa mwisho wa Kombe la Mapinduzi lililofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar na kufanikiwa kuingia Nusu Fainali kwa kuifunga Timu ya Mtibwa kwa mabao 2--1.
Benchi la Ufundi la Timu ya Mtibwa wakifuatilia mchezo wao na Tmu ya Yanga wakati wa michuano ya Kombe la Mapinduzi Timu ya Mtibwa imefanikiwa kuingia Nusu fainali kwa kushika nafasi ya Pili katika kundi lao kwa kufikisha pointi 4.
Kikosi cha Timu ya Yanga kilichoifunga Timu ya Mtibwa kwa mabao 2--1 wakati wa michuano ya Kombe la Mapinduzi mchezo uliofanyika usiku na kusubiri mshindi wa kundi B kati ya Timu ya Simba, JKU na URA ambazo zote zina nafasi ya kushika nafasi ya kwanza na ya Pili katika kundi hilo. 
Mshambuliajhi wa Timu ya Yanga akimpiga chenga beki wa timu ya Mtibwa wakati wa mchezo wao wa mwisho wa Kombe la Mapinduzi Timu ya Yanga imeshinda 2--1.
Mshambuliaji wa Yanga akijaribu kumpita beki wa Timu ya Mtibwa wakati wa mchezo wao wa Kombe la Mapinduzi mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar. 
Wachezaji wa Yanga na Mtibwa wakijiandaa kuzuiya mpira ukiwa juu wakati wa mchezo wao wa Kombe la Mapinduzi uliofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Yanga imeshinda mchezo huo kwa mabao 2--1.
Wachezaji wa Timu ya Yanga wakimsikiliza Kocha wao wakati wa mchezo wao na Timu ya Mtibwa. 
Wachezaji wa Timu ya Yanga wakiwa na mfugaji wa bao la kwanza la kusawazisha wakishangilia kwa aina yake.katika kipendera cha kona.
Beki wa Timu ya Mtibwa akiokoa mpira golini kwake na mshambuliaji wa Timu ya Yanga akiwa tayari kuchukua mpira huo.
Mchezaji wa Timu ya Mtibwa akimiliki mpira wakati wa mchezo wao wa Kombe la Mapinduzi.
Wachezaji wa Timu ya Yanga wakishangilia bao lao la ushindi dhidi ya Timu ya Mtibwa. .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.