Habari za Punde

"Yapo mengi ya kusema ila kwa leo nasema, pengo 

uliloliacha Mzee wetu Daniel Marwa Binagi tangu tarehe 06.02.2008 bado linaonekana na halitasahaulika kamwe. Mwenyezi Mungu Ailaze Roho yako Pahala Pema Peponi, Amina! Ni mimi mwanao Mpendwa

George Marwa Binagi (Pichani)".

Ilikuwa ni Sekunde, Dakika, Masaa, Siku, Wiki, Mwaka 

hatimae hivi sasa ni miaka Minane imepita tangu ututoke 

duniani Baba yetu Mpendwa, huku ukiacha kilio na majonzi 

kwa wanao tuliokuwa bado wachanga ambao hakika 

ulituacha ilihali tukihitaji malezi yako.

Ukiwa na Miaka 83 mwaka 2008, Mzee wetu Mzee Daniel 

Marwa Binagi Mzaliwa na Mkazi wa Kitongoji cha Chira Kata 

ya Turwa (Zamani), hivi sasa Kata ya Kenyamanyori Wilaya 

ya Tarime Mkoani Mara Mwenyezi Mungu alikupenda zaidi 

na kukuchukua ili ukapumzike baada ya kuteseka kwa 

maradhi katika kipindi cha muda mrefu.

Hakika uliipenda na kuiongoza Familia yako bila ubaguzi wa 

aina yoyote. Ulionyesha Mapenzi tele si tu kwa Wanao, 

Wajukuu zako, Wake zako bali kwa kila mmoja 

aliekuzunguka ambapo uliweza kuonyesha mapenzi tele 

kwake huku tabia yako ya kuchukia upuuzi na kuukumbatia 

ukweli ukikuongezea sifa rukuki kwa waliokufahamu.

Ukiwa na Elimu ya darasa la nne ambayo uliipata enzi za 

Mkoloni, uliweza kuleta mapinduzi ya ajabu katika Kijiji 

chako na hata Wilaya ya Tarime na kuwa mmoja wa Watu 

wenye Mafanikio makubwa Wilayani Tarime si tu kwa 

Kuwekeza katika Ujenzi wa nyumba na Biashara katika mji 

wa Tarime bali hata katika Uungwana wako.

Ulijizolea sifa ya kuhakikisha kila mtoto anapata elimu kadri 

apendavyo na hivyo ndivyo ilivyokuwa na ndiyo maana 

wakapatikana vijana mbalimbali kutoka katika uzao wako 

wakiwa nafasi mbalimbali za utumishi ikiwa ni pamoja na 

wale walioingia katika Sekta ya Elimu, Afya, Habari, 

Biashara, Urubani ikiwa ni miongoni mwa taaluma 

mbalimbimbali huku wewe mwenyewe ukiamini katika 

mfumo wa Biashara, Kilimo na Ufugaji.

Hakika wote waliopata malezi yako wanajivunia mpaka leo 

kuwa na Mzazi kama wewe Mzee wetu Daniel Marwa Binagi. 

Nakumbuka mambo mengi sana kutoka kwako ambayo 

ulikuwa ukiwatendea wakati huo mimi nikiwa mdogo. 

Nilitamani sana kupata malezi yako lakini Mwenyezi Mungu 

alikupenda zaidi. Nakumbuka namna ndugu zangu 

walivyosoma katika Shule na Vyuo vizuri tena kwa gharama 

kubwa. Naogopa kusema sana ili nisije nikakufuru ila nina 

kila sababu ya kusema kwamba pengine nami ningekuwa 

mmoja wa wanao ambao wangesoma katika shule na vyuo 

vizuri kama ulivyokuwa ukiniahidi wakati ukiwa kitandani 

unauguza maradhi yaliyokuwa yakikusibu.

Hakika Mzee wetu wetu Daniel Marwa Binagi tututaendelea 

kukukumbuka kwa kuyaendeleza yale yote mazuri 

uliyotuachia licha ya changamoto nyingi zinazojitokeza 

kutokana na pengo lako. Yapo mengi ya kusema ila kwa leo 

nasema kwamba pengo uliloliacha tangu tarehe 06.02.2008 

bado linaonekana na halitasahaulika kamwe. Hakika safari 

uliyoianza hapa duniani tangu tarehe 25.02.1925 ilifikia 

tamati mwaka huo wa 2008. Mwenyezi Mungu Ailaze Roho 

yako Pahala Pema Peponi, Amina! 


Ni mimi mwanao Mpendwa George Marwa Binagi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.