Mwanamuziki nyota nchini Vanes Mdee, akiweka dole gumba
tayari kuchapa kwenye fomu ya kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari, (PSS),
wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF wakati wa kongamano lililowakusanya wanafunzi wa
kike wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Shule ya Biashara na kufanyika chuoni
hapo mwishoni mwa wiki. Mamia ya wanachuo walijiunga na mpango huo baada ya
kupata elimu ya faida za kujiunga na mpango huo. Wanaoshuhudia, kutoka kulia ni
Balozi wa PSPF, Flaviana Matata ambaye ni mwanamitindo wa kimataifa anayefanya
kazi zake Ulaya na Marekani, Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, PSS wa
Mfuko huo, Mwanjaa Sembe, na Afisa Masoko na Uhusiano wa PSPF, Rahma Ngassa.
Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari (PSS), wa Mfuko wa
Pensheni wa PSPF, Mwanjaa Sembe, (aliyesimama), akizungumza kwenye kongamano la
wanafunzi wanawake wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (Shule ya Biashara), chuoni
hapo. Kushoto ni Balozi wa PSPF, Mwanamitindo wa Kimataifa anayefanya kazi zake
Ulaya na Marekani, Flaviana Matata
No comments:
Post a Comment