Katika kuelekea siku ya mwanamke
Duniani Kanisa la Living Water Centre Kawe kupitia huduma ya Wamama kanisani
hapo ikiongozwa na mmbeba maono Mwalimu Lilian Ndegi wameandaa Kongamano
linalojulikana kama “Kongamano la Moyo Wanawake”
Kongamano
hilo huwa linalofanyika mara moja kila mwaka Katika Kanisa la Living Water
Centre Kawe chini ya mtumishi wa Mungu Apostle Onesmo Ndegi na Mwalimu Lilian
Ndegi,Kongamano hili ni kwa kusudi la kuwajenga Wanawake kuwa na uwezo katika
kumtumika Mungu na kujua nafasi yao ya kutumika aliyowapa katika ufalme Mungu.
Theme ya mwaka huu ni Mwanamke Mjenzi
Mithali 14:1 Kusudi kuu la Kongamano ni Kuwafanya Wanawake kuwa watendaji
katika ufalme wa Mungu na wawajibikaji na watekelezaji wa majukumu katika ngazi
ya Familia,Huduma,Jamii na Taifa kwa ujumla.
Waimbaji Women of The Kingdom,Living
Waters,More than Enough Band na wengine wengi.
Karibuni sana.
Mawasiliano 0713 580 400
No comments:
Post a Comment