Habari za Punde

Balozi Seif Atembelea Maskani ya Kisonge Kujionea Uhariobifu Uliotokea Usiku wa Kuamkia leo.

Kikosi Maalum cha uchunguzi wa Miripuko cha Jeshi la Polisi Tanzania kinaendelea kufanya uchunguzi wa mripuko wa bomu uliotokea kwenye Kontena la Maskani ya Kisonge  iliyopo Mtaa wa Michenzani  Mjini Zanzibar.
Kikosi Maalum cha uchunguzi wa Miripuko cha Jeshi la Polisi Tanzania kinaendelea kufanya uchunguzi wa mripuko wa bomu uliotokea kwenye Kontena la Maskani ya Kisonge  iliyopo Mtaa wa Michenzani  Mjini Zanzibar.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambae pia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akifika eneo la tukio la mripuko wa Bomu Kisonge kueona hali halisi ya uharibifu uliotokea.Kulia ya Balozi Seif ni Katibu wa Chama cha Mapinduzi wa Maskani ya Kisonge Nd. Mzee Yunus.
Balozi Seif akiwapa pole Viongozi na Wanachama wa CCM Maskani Kaka ya Kisonge kufuatia mripuko wa bomu uliotokea kwenye Kontena lao jana usiku.
Picha na – OMPR – ZNZ.

Na Othman Khamis OMPR. 
Kikosi Maalum cha uchunguzi wa Miripuko cha Jeshi la Polisi Tanzania kinaendelea kufanya uchunguzi wa kina kufuatia mripuko wa bomu uliotokea kwenye Kontena na Maskani ya Chama cha Mapinduzi  ya Kisonge  iliyopo Mtaa wa Michenzani  Mjini Zanzibar majira ya saa sita usiku wa kuamkia leo.

Mripuko wa bomu hilo kwa hatua za awali linalokisiwa kutengenezwa kienyeji ulileta mtafaruk mkubwa kwa wakaazi wa eneo zima la nyumba za Maendeleo Michenzani pamoja na mitaa jirani.

Mmoja wa miongoni mwa watu walioshuhudia mripuko huo Bwana Shaaban Said alisema kwamba aliona kikundi cha vijana wasiopungua Sita waliovalia kanzu na vitambaa vyeupe kichwani  wakiwa ndani ya gari ndogo aina ya Keri wakionekana kulizunguuka Kontena hilo.

Bwana Shaaban alisema dakika mbili baadaye aliiona gari hiyo ikiondoka kwa mwendo wa kasi na kufuatia na mlio mkubwa wa mripuko pembezoni mwa Kontena hilo uliosababisha baadhi ya vioo vya madirisha ya nyumba za michenzani kupasuka pasuka.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM ambae pi ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alifika eneo la tukio hilo kujionea hali halisi ya tukio hilo la kusikitisha.

Katibu wa Maskani ya CCM Kisonge Ndugu Mzee Yunus alimueleza Balozi Seif  kwamba vipo baadhi ya vifaa vilivyoathirika kutokana na mripuko huo kwenye kontena hilo wanalolitumia zaidi kama stoo kwa ajili ya kuhifadhia vitu vyao licha ya kutofafanua zaidi gharama halisi iliyotokana na mripuko huo.

Nd. Yunus kupitia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliiomba Serikali kuimarisha zaidi ulinzi katika maeneo ya Umma ili kusaidia kupunguza matukio ya hujuma yanayofanywa na baadhi ya watu ambazo hujuma nyengine zina muelekeo wa chuki za Kisiasa.

Akitoa pole kwa Viongozi na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi Maskani Kaka ya Kisonge Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi alisema uchochezi huo wa hujuma haiufai na ni mbaya hasa wakati huu Taifa likielekea kwenye uchaguzi.

Balozi Seif alielezea masikitiko yake kutokana na vitendo hivyo vya kihuni vinavyofanywa na baadhi watu  katika baadhi ya maeneo hapa nchini ambavyo havitoi sura nzuri mbele ya uso wa Dunia.

Akiwa Mtendaji Mkuu wa Serikali aliviagiza Vyombo vya ulinzi kufanya uchaguzi wa kina wa tukio hilo la hujuma na kuwabaini wahusika wa tukio hilo ili wafikishwe kwenye vyombo vya  sheria.

Balozi Seif aliendelea kusisitiza kwamba nia ya Serikali zote mbili ile ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Mapinduzi ya Zanzibar  ni kuona kwamba Wananchi wote wanaishi katika hali ya amani na utulivu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.