Habari za Punde

Afisa Mdhamini, Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto Pemba akabidhiwa Ofisi

 ALIEKUWA Mkuu wa Idara ya maendeleo ya wanawake na watoto kutoka wizara ya wanawake na watoto Pemba, ambae kwa sasa ni Mkuu wa wilaya ya Chakechake Salama Mbarouk Khatib, akizungumza kwenye hafla ya kumkabidhi Afisa mdhamini mpya wa wizara hiyo, Khadija Khamis Rajab, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 WAFANYAKAZI wa wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto Pemba, waliohudhuria hafla ya kukukabidhiwa kwa Afisa Mdhamini mpya wa wizara hiyo, Khadija Khamis Rajab hayupo pichani, hafla iliofanyika wizarani hapo mjini Chakechake, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 AFISA Mdhamini wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto Pemba Khadija Khamis Rajab, akisaini hati ya makabidhiano mara baada ya kukabidhiwa wizara hiyo na aliekuwa mkuu wa Idara ya Maendeleo na wanawake na watoto wa wizara hiyo, Pemba Salama Mbarouk Khatib, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
AFISA Mdhamini wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto Pemba Khadija Khamis Rajab, akizungumza na watendaji wa wizara hiyo, muda mfupi mara baada ya kukabidhiwa wizara hiyo na aliekuwa mkuu wa Idara ya Maendeleo na wanawake na watoto wa wizara hiyo, Pemba Salama Mbarouk Khatib, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.