Habari za Punde

Benki ya TIB yaendesha mafunzo ya bure ya ujasiriamali Sabasaba

 Mkufunzi wa Mafunzo ya Ujasiriamali  yanayoendeshwa na benki ya TIB katika viwanja vya Sabasaba, Louis Mkuku, akitoa mafunzo kwa baadhi ya wahudhuriaji wa semina hizo zinazoendelea katika viwanja vya Sabasaba.
 Baadhi ya wafanyabiashara wakifatilia mafunzo ya uajasiriamali yanayoendeshwa na benki ya TIB katika viwanja Sabasaba.
 Mkufunzi wa Mafunzo ya Ujasiriamali yanayoendeshwa na benki ya TIB katika viwanja vya Sabasaba, Louis Mkuku, akitoa mafunzo kwa baadhi ya wahudhuriaji wa semina hizo zinazoendelea katika viwanja vya Sabasaba.

Mkufunzi wa Mafunzo ya Ujasiriamali yanayoendeshwa na benki ya TIB katika viwanja vya Sabasaba, Louis Mkuku, akitoa mafunzo kwa baadhi ya wahudhuriaji wa semina hizo zinazoendelea katika viwanja vya Sabasaba.
Benki ya TIB kwa kushirikiana na Taasisi ya Ujasiriamali na Uongozi wa Biashara (IMED) wanaendesha mafunzo ya bure ya ujasiriamali katika banda la TIB lilipo katika viwanja vya Sabasaba.

Mafunzo hayo pia yanajumuisha elimu katika maeneo ya uongozi na sheria za biashara, masoko, utawala wa fedha pamoja na utawala wa biashara yanalenga wajasiriamali wadogo wadogo na wa kati ili kuwajengea uwezo wa kukuza biashara zao.

Akizungumzia mafunzo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TIB, bwana Charles Singili, alisema wameamua kutoa mafunzo hayo katika msimu huu wa Sabasaba ili kuwafikia wafanyabiashara wengi zaidi pamoja na wananchi wa kawaida.

‘Mafunzo haya ni bure, na yanafanyika katika banda letu la TIB hapa Sabasaba na wananchi wote wanakaribishwa kuja kujifunza ili waweze kuendesha biashara zao kwa faida na mafanikio’ alisema bwana Singili.

Mafunzo hayo ambayo yamejikita katika kuwapa wafanyabiashara mbinu za kuendesha miradi yao pamoja na kutumia vizuri mikopo inayotolewa na benki hiyo yanafanyika kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa saba mchana, na yataendelea hadi tarehe 4 ya mwezi Julai.

‘Kimsingi mafunzo haya yanaendana na dhima ya mwaka huu ya maonyesho ya Sabasaba, Kuunganisha Uzalishaji na  Masoko, na hivyo kwa elimu tutakayowapa wajasiriamali tunaamini wataweza kupanua wigo wa masoko ya biashara zao’ alimaliza bwana Singili.

Naye mmoja wa wanufaika wa elimu hiyo, daktari Bayoum Awadh,kutoka kampuni ya Emergent Africa, aliipongeza benki ya TIB kwa kutoa mafunzo hayo kwani yatazidi kuwaongezea elimu na uzoefu zaidi wa kuendesha biashara zao.

‘Naishukuru sana benki ya TIB kwa kuendesha mafunzo haya, na nawaomba wajasiriamali wenzangu wajitokeze kwa wingi kujipatia elimu hii kwani itawasaidia sana kuendesha biashara zao kwa faida’ alisema daktari Bayoum Awadh.No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.