Habari za Punde

Kampuni ya Simu ya ZANTEL Yakabidhi Hundi kwa Kikundi cha Ushirika Kisiwani Pemba

Mkurugenzi biashara wa Zantel- Zanzibar, Ndg.Ibrahim Atas, akielezea jambo kwenye hafla ya kukakabidhi hundi ya shilingi million 5, kwa wanakikundi cha ‘nia ni umoja’ cha Kangani wilaya ya Mkoani, hafla iliofanyika makao makuu ya kampuni hiyo Chakechake Pemba
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Zantel Benoit Janin, akizungumza kabla ya kampuni yake kuwakabidhi hundi ya shilingi milion 5 wanakikundi cha ‘nia ni umoja’ cha Kangani wilaya ya Mkoani, hafla hiyo ilifanyika ofisi za Zantel Chakechake Pemba
Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel Benoit Janin, akimkabidhi Mwenyekiti wa kikundi cha ‘nia ni umoja’ Khamis Kombo Iddi, hundi ya shilingi milion 5, katikati ni Afisa kiliomo wilaya ya Mkoani, Amini Rashid Mdowe


Mwenyekiti wa Kikundi cha ‘Nia Ni Umoja’ Ndg.Khamis Kombo Iddi, akitoa neneo la shukurani, kwa uongozi wa kampuni ya Zantel, baada ya ushirika wake kukabidhiwa hundi ya shilingi milion 5, katikati ni Afisa kilimo wilaya ya Mkoani Pemba, Amini Ubwa Mdowe, na kushoto ni Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo Benoit Janin
Baadhi ya wanakikundi cha ‘nia ni umoja’ cha Kangani wilaya ya Mkoani Pemba na waandishi wa habari, wakiwa kwenye hafla ya kukabidhiwa hundi ya shilingi milion 5 kutoka kwa kampuni ya Zantel, kwa ajili ya kuendeleza ushirika wao upandaji migomba, hafla hiyo ilifanyika mjini Chakechake Pemba
Baadhi ya wanakikundi cha ‘nia ni umoja’ cha Kangani wilaya ya Mkoani Pemba na waandishi wa habari, wakiwa kwenye hafla ya kukabidhiwa hundi ya shilingi milion 5 kutoka kwa kampuni ya Zantel, kwa ajili ya kuendeleza ushirika wao upandaji migomba, hafla hiyo ilifanyika mjini Chakechake Pemba
Afisa kilimo Wilaya ya Mkoani Pemba, Amini Rashid Mdowe, akielezea changamoto zinazowakabili wakulima wa Pemba, kwenye hafla ya kukabidhiwa kwa hundi ya shilingi milion 5, iliotolewa na kampuni ya simu ya Zantel, kwa ushirika wa ‘nia ni umoja’ hafla iliofanyika afisi ya kampuni hiyo Chakechake Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.