Habari za Punde

Timu ya Vijana ya Wilaya ya Mjini Yaagwa Kuelekea Arusha Kushiriki Mashindano ya Rolling Stone.

 Afisa Habari wa ZFA Ali Cheupe akitowa maelezo kabla ya kuaza kwa hala ya kuiaga Timu ya Vijana ya Wilaya ya Mjini Unguja inayokwenda Arusha kushiriki michuano ya Rolling Stone. hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa VIP Uwanja wa Amaan Zanzibar.Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe Rashid Ali Juma akizungumza na Wachezaji wa Timu ya Vijana ya Wilaya ya Mjini Unguja wakati wa kuiaga timu hiyo na kuwataka kuonesha uhodari wao na kuiletea heshima Zanzibar katika mchezo wa mpira wa miguu.
Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Mhe Rashid Ali Juma akimkabidhi seti ya jezi Mshauri wa Wizara ya Habari Zanzibar Mhe Abdalla Mwinyi Khamis kwa ajili ya kuwakabidhi Wachezaji wa Timu ya Vijana ya Wilaya ya Mjini Unguja, hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika ukumbi wa VIP Uwanja wa Amaan Zanzibar, anayeshuhudia ni Mshauri wa Rais Utamaduni Mhe Chimbeni Kheri.
MSHAURI wa Rais Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis akimkabidhi seti ya jezi Nahodha wa Timu ya Wilaya ya Mjini Unguja Ibrahim 
Mohammed, wakati wa kuagwa kwa timu hiyo inayoshiriki michuano ya Roling Stone yanayofanyika Mkoani Arusha, hafla hiyo imefanyika ukumbi wa VIP Uwanja wa Amaan 
Zanzibar.katikati Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Mhe Rashid Ali Juma
MSHAURI wa Rais Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis akimkabidhi mpira  Nahodha wa Timu ya Wilaya ya Mjini Unguja Ibrahim Mohammed, wakati wa kuagwa kwa timu hiyo inayoshiriki 
michuano ya Roling Stone yanayofanyika Mkoani Arusha, hafla hiyo imefanyika ukumbi wa VIP Uwanja wa Amaan Zanzibar.katikati Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Mhe Rashid Ali JumaNo comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.