Habari za Punde

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Waichangia Timu ya Vijana ya Wilaya ya Mjini Unguja Kushiriki Michuano ya Roling Stone Arusha.


Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Mhe Rashid Ali Juma akizungumza na Wachezaji na Viongozi wa Timu ya Wilaya ya Mjini Unguja walipofika katika Jengo la Baraza la Wawakilishi Zanzibar kujitambulisha kwa Wajumbe na kupokea Mchango uliochangwa na Wajumbe wa Baraza kuiwezesha timu hiyo kushiriki katika michuano ya Roling Stone yanayofanyika Mkoani Arusha wiki hii. Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wameishangia Timu hiyo fedha kwa ajili kuweza kushiriki vizuri michuano hiyo.kulia Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Mhe. Mohammed Ahamad na Naibu Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Mhe Chuom Kombo.
Mwenyekiti wa ZFA Wilaya ya Mjini Ndg. Hassan Chura wakiwa katika hafla hiyo wakimsikiliza Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Mhe Rashid Ali Juma akitowa nasaha zake kwa Viongozi hao na Wachezaji wakati wa hafla ya kukabidhiwa fedha waliochangiwa na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni na Kiongozi wa Timu ya Baraza la Wawakilishi Sport Club Mhe Nassor Jazira akitowa nasaha zake kwa Wachezaji wa Wilaya ya Mjini wanaokwenda Arusha kushiriki michuano ya Roling Stone kuiwakilisha vizuri wilaya yao na kurudi na ushinda. 
Kiongozi wa Timu ya Baraza la Wawakilishi Sport Club na Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni Mhe. Nassor Salum Jaziri akikabidhi mchango uliotolewa na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kwa Mwenyekiti wa ZFA Wilaya ya Mjini Ndg Hassan Chura, kwa ajili ya timu hiyo kuweza kushiriki vizuri katika michuano hiyo inayofanyika Mkoani Arusha mwishoni mwa wiki hii.

Wachezaji wa Wilaya ya Mjini Unguja wakimsikiliza Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Mhe Rashid Ali Juma akitowa nasaha zake kwa wachezaji hao kuweza kushiriki vizuri michuano hiyo. 
Kocha wa Timu ya Wilya ya Mjini King akiwa na Wachezaji wake wakati wakitambulishwa kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakati wa kukabidhiwa fedha zao zilizochangwa na Wajumbe. 
Mwakilishi wa Jimbo la Jangombe akiwasikiliza Viongozi wa Timu ya Wilaya ya Mjini walipofika katika jengo la Baraza Chukwani kujitambulisha.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akiwa katika picha ya pamoja na Wachezaji wa Timu ya Wilaya ya Mjini walipofika katika mjengo wa Baraza la Wawakilishi Chukwani kujitambulisha na kuwaaga wakielekea Mkoani Arusha kushiriki michuano ya Roling Stone. 
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Simai Mohammed Said (Mpaka basi) akizungumza na wachezaji wa timu ya Wilaya ya Mjini Unguja walipofika kujitambulisha kwa Wajumbe wa Baraza na kukabidhiwa fedha za mchango waliochanga waheshimiwa wawakilishi kwa ajili ya timu hiyo.
Wachezaji wa Timu ya Wilaya ya Mjini wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakiwa nje ya jengo hilo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.