Habari za Punde

Rais wa Zanzibar Dk.Shein Atembelea Ukumbi wa Baraza la Eid Fitr Kikwajuni Zanzibar.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe,Haruna Ali Suleiman wakati alipotembelea Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wa Zamani,Vuga Mjini Unguja ambao unatarajiwa kufanyika kwa Baraza la Eid el Fitri linalofanyika  kila mwaka baada ya mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe,Haruna Ali Suleiman (kushoto) na Katibu Mkuu Ofisi ya makamo wa Pili wa Rais Joseph Abdalla Meza(kulia)  wakati alipotembelea Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wa Zamani,Vuga Mjini Unguja ambao unatarajiwa kufanyika kwa Baraza la Eid el Fitri linalofanyika  kila mwaka baada ya mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,[Picha na Ikulu.]STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
  Zanzibar                                                            1.07.2016
---
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo ametembelea ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani uliopo Kikwajuni mjini Unguja ambao umefanyiwa ukarabati mkubwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Dk. Shein alipokelewa na viongozi mbali mbali wa Serikali waliofika katika eneo la ukumbi huo na baadae alipata maelezo mafupi juu ya ukarabati huo mkubwa uliofanywa ambao utaanza kutumika kwa ajili ya Baraza la Idd-el Fitri baada ya kumaliza mwezi mtukufu wa Ramadhan unaoendelea mwaka huu.

Akitoa maelezo mafupi juu ya ukarabati huo kwa Rais wa Zanzibar, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Joseph Abdulla Meza  alisema kuwa tayari ukarabati wa ukumbi huo umeshakamilika na uko tayari kwa kutumika.


Alisema kuwa ukarabati huo ulianza mwanzoni mwa mwezi uliopita chini ya mafundi kutoka Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ kupitia vikosi vyake vya KMKM na Chuo cha Mafunzo pamoja na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji ambapo mafundi wake wamekarabati eneo la mbele la ukumbi huo kwa kutia lami.

Katibu Meza aleleza kuwa ukarabati huo pia ulihusisha ukumbi huo wa Baraza la Wawakilishi la zamani, vyoo, kuweka paa jipya, silingi, mazulia, upakaji rangi pamoja na kutia vifaa vyengine mbali mbali vipya.

Nae Dk. Shein kwa upande wake alipongeza juhudi zilizochukuliwa katika ukarabati huo pamoja na sehemu nyengine muhimu huku akiahidi kuwa Serikali itaendelea kuuimarisha zaidi ukumbi huo.

Ukumbi huo unatarajiwa kutumika kwa mara ya kwanza kwa ajili ya Baraza la Idd- el- Fitri ambalo linatarajiwa kufanyika wiki ijayo na baadae utaendelea kutumika kwa shughuli mbali mbali za kiserikali pamoja na matumizi mengine kadri serikali itakavyoona inafaa.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

1 comment:

  1. Serikali ilokuwa haina vison!! Kutumia pesa kwa kuimasharisha vitu ambavyo tija yake kwa jamii ni ndongo! Airport ya Zanzibar iko hali mbaya sana ambayo ni moja ya vitu ambavyo Dunia nzima vinapewa kipa umbele lakini pia ni moja kati vitu vinavyoleta tija kwa wananchi!! Badara ya zanzibar tumeona msongomano wa makontena na pia wamiliki wa meli za mizigo kulalamikia kukaa nje ya port kwa muda kabla ya kuweza kushusha mizigo!! Baraza la idi ukumbi wa Salama si upo???

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.