Baraza la vyama vya mpira wa miguu kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati limekiri muamuzi aliyechezesha pambano kati ya Zanzibar Queen dhidi ya Burundi kuchemsha kwenye maamuzi yake.
Carolyne Wanjala kutoka nchini Kenya alitoa alishindwa kuitafsiri sheria namba 12 ya mchezo wa soka kwa kumtoa nje mlinda mlango namba moja Amina Mohammed kwa madai ya kuudaka mpira nje ya eneo.
Ripoti iliyotumwa kwa kamati ya mashindano imeonyesha kuwa muamizi huyo alishindwa kutoa maamuzi sahihi kwa alipaswa kutoka kadi ya njano badala ya nyekundu.
Kitendo hicho ambacho kiliwashangaza wengi kimewafanya viongozi wa CECAFA kuingia kwenye lawama kwa kuchukua waamuzi ambao hawana viwango.
Zanzibar Queen watashuka tena dimbani kesho saa kumi alasiri kucheza na wenyeji Uganda lakini kpambano hilo litatanguliwa na mchezo wa saa nane kati ya Kenya dhidi ya Burundi.
No comments:
Post a Comment