Habari za Punde

Wingi wa Zanzibar Queen AQendelea Kupata Matibabu Rippon Jinja.

Na Mwandishi Wetu Jinja Uganda.

Madaktari bingwa wa kituo cha huduma za afya cha Rippon kiliopo Jinja nchini Uganda wanaendelea kutoa huduma kwa mchezaji wa Zanzibar Queen aliyeumia kwenye mchezo wa jana dhidi ya wenyeji Uganda.
Siajab Hassan Ali anayechezea timu ya Women Fighter alizimia kiwanjani Mara baada ya kukwatuana na mshambuliaji wa Uganda kwenye heka heka za kuokoa mpira.


Daktari wa timu Mwanahamis Othman kwa kushirikiana na vijana wa msalaba mwekundu uwanjani Njeru, walijaribu kutoa huduma ya kwanza lakini mchezaji huyo hakuweza kuzibdukana uwanjani hapo.


Wasimamizi wa mashindano hayo CECAFA waliamuru gari la kubebea wagonjwa kiwanjani hapo kumpeleka mchezaji huyo hospitalini hapo.

Jioni ya leo mchezaji huyo anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi (x-ray) kwenye mguu wake wa kushoto ambao umeonekana kupata dhoruba kali.

Mashabiki wa soka nchini hapa waliitaja siku ya jana kuwa ya kihistoria kwenye mashindano hayo ya Cecafa kwa timu za taifa za Wanawake kutokana na kuwa na majeruhi wengi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.