Habari za Punde

Wizara ya Mambo ya Nje yakabidhi Msaada kwa Waathirika wa Tetemeko la Ardhi Mkoani Kagera.

Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akipokea mfano wa hundi ya Shilingi milioni 10 kutoka kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (katikati) ikiwa ni mchango wa Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera hivi karibuni. Mkutano huo wa kuhamasisha uchangiaji  ulifanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 13 Septemba, 2016 na kuwashirikisha Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini na Wafanyabiashara. Kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Charles Mwijage na kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Aziz Mlima
Sehemu ya Mabalozi na Wafanyabiashara walioshiriki mkutano huo
Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa akitoa hotuba wakati wa mkutano wa kuhamasisha uchangiaji kwa maafa yaliyotokea Kagera kufuatia tetemeko la ardhi.
Sehemu nyingine ya wafanyabiashara akiwemo Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Dkt. Reginald Mengi (wa kwanza kushoto)
Sehemu ya wageni waalikwa walioshiriki mkutano huo wakiwemo Wakurugenzi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Mhe. Dkt. Kolimba akitoa neno la ukaribisho wakati wa mkutano huo
Mwenyekiti wa TPSF, Dkt. Mengi akizungumza wakati wa mkutano huo.
Mkutanoo ukiendelea

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.