TIMU ya 34 ya Madaktari Bingwa kutoka Jamhuri ya Watu wa China wamewafanyia uchunguzi wa afya Watoto wa Nyumba wa Watoto Yatima Mazini Zanzibar na kuwapatiwa huduma za afya na kuwafanyika uchunguzi wa afya zao.
Akizungumza mara baada ya kuwapatia huduma watoto hao Kiongozi wa Madaktari wa timu ya 34 kutoka China Dr.Wei Chen amesema jumla ya watoto 60 wamepatiwa huduma na wataendelea kuisaidia sekta ya Afya katika nyanja tofauti ikiwemo kuwapatia huduma wananchi wa visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na watoto wenye mahitaji maalumu.
Amefahamisha kuwa watoto wanaolelewa kituo Cha Mazizini na vituo vyengine wanahitaji kuchunguzwa afya zao mara kwa mara endapoa watakuwa na matatizo ya kiafya waweze kuhudumiwa na kuondokana na maradhi na waweze kuishi kwa furaha katika maisha yao.
Amesema Serikali ya China itaendelea kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha huduma mbali mbali ikiwemo sekta ya Afya kwa kutoa huduma katika maeneo mbalimbali hapa nchini, kuwajengea uwezo wataalamu pamoja kusaidia dawa na vifaa tiba.
Mkuu wa Kituo cha Watoto Yatima Mazizini Zanzibar Wahida Abdalla Hassan amefurahishwa na ujio wa madaktari hao kwa kuwahudumia watoto katika kituo hicho na kuwafanyika vipimo mbalimbali na kuwapatia matibabu.
Aidha ameiomba timu ya madaktari kutoka China kuendelea kuwapatia huduma hiyo watoto hao katika kituo hicho ili kuondokana na maradhi mbali mbali.
Timu ya 34 ya madaktari kutoka China imekuwa na kawaida kutoa huduma na kufanya uchunguzi wa maradhi mbalimbali kwa wananchi wa makundi maalumu kwa kuwafata katika maeneo yao.
No comments:
Post a Comment