· Redio jamii Pemba zaibuka kidedea kwa kuendeleza misingi ya usawa wa kijinsia, wakifuatiwa na gazeti la Zanzibar Leo
· Asya Hassan wa Zanzibar Leo aibuka
mshindi wa Jumla
· Waandishi chipukizi nao wang’ara.
Jumla
ya waandishi wa habari wanane (8) na vyombo vya habari vitatu (3) wameibuka
kidedea katika tuzo za Umahiri za Uandishi wa Habari za Takwimu za wanawake
na uongozi zilizoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake
Tanzania, Zanzibar (TAMWA ZNZ) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa
Serikali (OCGS) pamoja na Jumuiya ya Wanawake wenye Ulemavu Zanzibar (JUWAUZA),
Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) na Jumuiya ya Mazingira,
Jinsia na Utetezi Pemba (PEGAO).
Miongoni mwa vipengele vilivyoshindaniwa
ni kipengele cha radio, kipengele cha magazeti, kipengele cha mitandao ya
kijamii, kipengele cha waandishi wa habari vijana (YMF) na kipengele cha vyombo vya habari vyenye kuendeleza na
kukuza usawa wa kijinsia.
Kati ya washindi hao wanane,
watano miongoni mwao walitoka katika
kipengele cha waandishi wa Habari vijana ambao walitambuliwa kwa kuzawadiwa vyeti pamoja na iPad kwa kila
mmoja. Washindi hao ni:
- Salum Ameir Salum
- Zurima
Ramadhan
- Nihifadhi
Abdulla Issa
- Fatma
Hamad Faki
- Maryam
Nassor Suleiman
Vilevile, Asya Hassan Bakar kutoka
gazeti la Zanzibar Leo aliibuka kuwa mshindi wa jumla na mshindi katika kipengele
cha gazeti, alizawadiwa cheki ya shilingi Milioni moja na Laki tano,
cheti
pamoja na trofi, mwengine ni Huwaida
Nassor Moh’d kutoka Assalam Fm Radio ambae amekua mshindi wa kwanza katika
kipengele cha Redio nae
alizawadiwa cheki ya Shilingi milioni
moja, cheti
pamoja na trofi na mshindi wa
kwanza katika kipengele cha mitandao ya kijamii ni Salum Ameir Salum alipokea cheki ya Shilingi milioni moja, cheti pamoja na trofi
Kwa upande wa Vyombo vya Habari jumla ya vyombo
vitatu vya habari vilitambuliwa
kwa juhudi zao katika kuendeleza na kukuza usawa wa kijinsia kwenye kazi zao za
kila siku, vyombo hivyo vilizawadiwa cheki ya Shilingi milioni mbili
(2,000,000) kwa kila kimoja pamoja na vyeti vya shukran. Vyombo vya habari
vilivyoibuka washindi ni:
- Redio Jamii Micheweni.
- Redio Jamii Mkoani.
- Shirika la Magazeti ya Serikali.
Waandaaji
wa Tuzo hii wanatoa wito kwa waandishi wa habari wa na vyombo vya Habari
kuendelea kuandika habari zinazohusu takwimu za wanawake na uongozi, kusimamia
na kukuza usawa wa kijinsia, kuelezea mazuri yanayofanywa na wanawake na vikwazo
mbalimbali vinavyowazuia wanawake wasifikie nafasi za uongozi.
Jumla
ya kazi 235 kutoka vyombo vya habari vya aina zote vikiwemo magazeti, redio,
televisheni pamoja mitandao ya kijamii, ziliwasilishwa kwa ajili ya
kushindanishwa, ambapo jumla ya kazi 120 zilikabidhiwa kwa majaji kwa ajili ya
kufanyiwa uchambuzi na hatimae kupatikana washindi hao.
Tuzo
hizi ni sehemu ya utekelezaji wa programu ya Kuwawezesha Wanawake kushika
nafasi za uongozi (SWIL), ambayo inatekelezwa na Chama cha Waandishi wa
Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA ZNZ), Jumuiya ya Wanawake wenye
Ulemavu Zanzibar (JUWAUZA), Jumuiyay a Mazingira, Jinsia na Utetezi Pemba (PEGAO)
na Jumuiyay a Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA), kwa ushirikiano na Ubalozi
wa Norway nchini Tanzania.
Imetolewa na:
TAMWA ZNZ, JUWAUZA, ZAFELA & PEGAO.
No comments:
Post a Comment