Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad
Yussuf Masauni akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mazingira wa Serikali
ya Japan Mhe. Asao Keiichiro (Kei) wakati wa hafla ya utiaji saini wa Hati ya
Makubaliano ya ushirikiano katika mpango wa pamoja wa uwekezaji katika Biashara
ya Kaboni utakaowezesha kampuni za nchi hizo mbili kuwekeza katika Biashara ya
Kaboni nchini Tanzania, iliyofanyika Mei 28, 2025 Tokyo, Japan.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja na kushoto akiteta jambo
na Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria Ofisi ya Makamu wa Rais Bw.
Dustan Shimbo wakati wa hafla ya utiaji saini wa Hati ya Makubaliano ya
ushirikiano katika mpango wa pamoja wa uwekezaji katika Biashara ya Kaboni
utakaowezesha kampuni za nchi hizo mbili kuwekeza katika Biashara ya Kaboni
nchini Tanzania, iliyofanyika Mei 28, 2025 Tokyo, Japan. Kushoto ni Dkt.
Shirima kutoka Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC).
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad
Yussuf Masauni akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini wa Hati ya
Makubaliano ya ushirikiano katika mpango wa pamoja wa uwekezaji katika Biashara
ya Kaboni utakaowezesha kampuni za nchi hizo mbili kuwekeza katika Biashara ya
Kaboni nchini Tanzania, iliyofanyika Mei 28, 2025 Tokyo, Japan.
Akizungumza mara baada ya utiaji saini huo, Waziri Masauni amesema Makubaliano ya Mashirikiano yaliyosainiwa yamekusudiwa kuimarisha uhusiano kati ya Japan na Tanzania kwa maendeleo endelevu na hatua za kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi.
Alisema ushirikiano huu utaongeza fursa ya kupanua soko la Biashara ya Kaboni kutoka kwa wawekezaji wa Japan watakaowekeza katika miradi ya biashara ya Kaboni itakayoibuliwa nchini.
Waziri Masauni alieleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan anawataka wataalamu kutoka nchi hizi mbili kufanya kazi haraka, kwa bidii na kwa pamoja kwa manufaa ya nchi zote mbili ili kuhakikisha kuwa makubaliano hayo yanakwenda katika hatua ya utekelezaji.
"Tuko tayari kufanya kazi kwa ukaribu na wenzetu wa Japan ili kuhakikisha makubaliano haya yanatekelezwa kwa faida ya nchi zote mbili. Tayari Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeimarisha uwezo wa kitaasisi na kisheria katika usimamizi wa Biashara ya Kaboni ambapo Ofisi ya Makamu wa Rais iliandaa kanuni za mwaka 2022 za kuratibu biashara ya Kaboni”, alisisitiza Mhe. Masauni.
Aidha, Mhandisi alibainisha kuwa katika Mfumo wa Kitaasisi, Serikali imeanzisha Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC) kupitia Sheria ya Usimamizi wa Mazingira iliyofanyiwa marekebisho ya 2025.
No comments:
Post a Comment