Habari za Punde

Waziri Hamad Rashid: Tumejipanga kwa kila mwezi kutembelea Pemba pasi na taarifa


Na Salmin Juma - Pemba

Waziri wa kilimo, maliasili mifugo na uvuvi  Zanzibar Mh Hamad Rashid Mohammed amesema kua wizara yake imejipanga kikamilifu kwa kila mwezi kupata siku maalum za kutembelea kisiwa cha Pemba pasi  na taarifa kama ilivyozoeleka ikiwa lengo ni  kukagua harakati za kimaendeleo  zilizotakiwa kufanywa  na wizara hiyo, ni kwa kiwango gani zinatekelezwa na maafisa wake.

Amesema ili kujua ufanisi wa kazi  kwa maafisa wa wizara hiyo Pemba kuanzia yeye, katibu mkuu na viongozi wengine katika wizara yake wapotayari kutekeleza suala hilo.

Mh: Hamad Rashid ameyasema hayo leo katika ziara maalum iliyoanzia  Weni mkoa wa kaskazini Pemba alipokua akiwakabidhi mapikipiki mabwana na mabibi shamba kwa lengo la kuwatatulia adhaa iliyokuwa ikiwakabili katika kuwafikia wakulima, wafugaji na wananchi kwa ujumla wenye uhusiano wa harakati zao na wizara hiyo.

Amesema wakulima na wafugaji katika maeneo mbalimbali wa kisiwani Pemba  wanakabiliwa na changamoto tofauti katika kazi zao, hivyo kupitia usafiri huo wa mapikipiki amewataka maafisa hao kujibidiisha katika kuwafikia kila mkulima au mfugaji atakaefikwa na tatizo au hata kuwatembelea tu ili kujua shida zinazowakabili.

Hamad

amesema mapikipiki hayo ni sharti yatumike katika lengo lililokusudiwa na si kinyume chake, huku akisema hakutokua na muhali kwa yoyote yule atakae tumia Honda hizo kwa maslahi yake binafsi ambayo yataonekana kua hayana manufaa kwa wizara.



“kuna orodha  ya watu ambao waliwahi kupewa pikipiki  lakini wamezificha wanataka kuziuza na hata waliyopewa boti wapo wanaotaka kufanya ubadhirifu lakini hilo linashughulikiwa”alisema Hamad.

Jumla ya pikipiki kumi na nane(18) zilizogharimu shilingi milioni khamsini na tisa zilitolewa kwa maafisa hao wakiwamo akina mama watano.

Katika kutilia mkazo suala la kufanya kazi kwa bidii dhidi ya mabwana na mabibi shamba pamoja na maafisa kilimo na ufugaji waziri Hamad Rashid amsema, atakua na utaratibu maalum wa kuchuguza utendeji kazi  ambapo amesema  atamuuliza kila mmoja wapi alipotembelea huku akitaka kuonyeshwa buku lenye litakalo ashiria wapi  alipokwenda na nini  alichokifanya.

Mh pia alibahatika kutembelea kikundi sha urishika cha “Umoja ni nguvu” Vikunguni, ambacho kinajishuhulisha na ufugaji wa Ng’ombe wa maziwa wa kisasa ambapo amepongeza kazi hiyo huku akiwataka wanakikindi hicho kuzidisha nguvu ili kufikia lengo la  kujikwamua kimaisha na hata seriakili kunifaika kutoka kwao.

Aidha ametoa rai ya kutafuta ng’ombe wa kienyeji kuwafuga pamoja kwani  wanathamani kubwa sana na wataweza kuwaingizia kupato chakutosha na hatimai kuinua mradi wao huo.

Waziri huyo wa kilimo, maliasili, mifugo na uvuvi pia ametembelea katika kikundi cha ufugaji  Ngombe Kinyasini, kikundi cha upandaji miti na uhifadhi mazingira (UMUMA) pia ametembelea sehemu maalum itakayo jengwa kiwanda cha samaki Jimbumbwana Kangagani na kwengineno.

Ziara hiyo ilikua ni mkoa wa kaskazini Pemba ambapo siku ya Jumanne ya tarehe 13/09/2016 ziara hiyo itaendelea tena katika mkoa wa kusini Pemba ikiwa lengo ni kuwatembelea, kuwakagua na kusikiliza faida na changamoto zinazopatika kutoka kwa wakulima na wafugaji kisiwani Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.