Habari za Punde

Bunge la Afrika Mashariki Kufanyika Zanzibar Kesho Katika Ukumbi wa Jengo la Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

Jengo la Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar linalotarajiwa kufanyika kwa Mkutano wa Bunge la Afrika Mashariki kesho tarehe 11-10-2016 kwa muda wa wiki mbili. Bunge hilo linafanya mkutano wake hii ikiwa ni mara ya pili kufanyika Zanzibar mkutano wa mwanzo uliofanyika mwaka 2007.
Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar unaotarajiwa kufanyika kwa Mkutano wa Bunge la Afrika Mashariki kesho. 
Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Hon Daniel Fred Kidega, akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar na kutoa taarifa ya kukamilika kwa maandalizi ya Mkutano huo hapo kesho kulia Mbunge wa Afrika Mashariki kutoka Tanzania Mhe Makongoro Nyerere na kushoto Mbunge wa Afrika Mashariki kutoka Nchini Rwanda Mhe. Patricia Hajabakiga.
Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Hon Daniel Fred Kidega, akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar kuhusiana na kuaza kwa Mkutano wa Bunge la Afrika linalotarajiwa kufanyika kesho katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar. kulia Mbunge wa Bunge hilo Mhe. Makongoro Nerere, mkutano huo na waandishi umefanyika katika ukumbi wa baraza chukwani leo mchana. 
Baadhi ya Wabunge wa Afrika Mashariki wakimsikiliza Spika wa Bunge hilo wakati akiongea na waandishi wa habari kukamilika kwa matayarisho ya mkutano huo hapo kesho.
Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki wakati akitoa taarifa ya mkutano huo kwa waandishi wa habari Zanzibar.
Baadhi ya Wabunge wa Afrika Mashariki wakifuatilia mkutano huo na waandishi wa habari Zanzibar.Mwandishi akiuliza swali wakati wa mkutano huo na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki.
Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Hon Daniel Fred Kidega akijibu maswali alioulizwa na waandishi wakati wa mkutano huo. 


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.