Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Azungumza na Waziri Mkuu wa Tanzania.

Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa kushoto akimkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Nyumbani kwake Mtaa wa Osterbay Jijini Dar es salaam.
Viongozi hao ambao ndio watendaji Wakuu wa Serikali za SMT na SMZ wamekuwa na utaratibu wa kukutana kila baada ya kipindi kubadilishana mawazo ya kiutendaji baina ya pande hizo mbili za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mratibu Mkuu wa Ofisi ya Uratibu wa Shughuli za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar {SMZ} Dar-es-salaam Ndugu Issa Mlingoti Ali.(Picha na – OMPR – ZNZ.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.