Habari za Punde

Masheha Kisiwani Pemba Watakiwa Kuwahamasisha Wananchi Kushiriki Utoaji wa Dawa za Matende.

Na Salmin Juma kutoka Pemba
Masheha kisiwani pemba wametakiwa kuwahamasisha wananchi kujitokeza kushiriki kampeni ya utoaji wa dawa za matende, minyoo na kichocho ambalo linaatrajia kuanza kutekelezwa ya jumamosi ya oktoba 30-hadi jumapili ya 31 mwaka huu .

Mkuu wa kitengo cha kichocho pemba salehe juma mohammed amesema ili kufanikisha kampeni hiyo kunahitajika uhasishaji wa kutosha pamoja na ushiriki wa masheha katika maeneo yao ya uongozi .

Kauli hiyo ameitoa kwa nyakati tofauti wakati akizungumza na masheha wa Wilaya ya wete na Micheweni akiwa katika ziara yake ya kuhamasisha viongozi wa serikali za shehia kutoa msukumo kwa wananchi wao .

Amesema kwa upande wa watendaji wa kitengo hicho pemba wamekuwa wakitoa elimu na hamasa kwa wananchi kupitia skuli , madrasa pamoja na kwenye mikusanayiko ya watu hali ambayo imeongeza elimu kwa wananchi .

Aidha amewasisitiza wananchi kuhakikisha dawa wanazopatiwa wanazitumia pale pale baada ya kupewa ili ziweze kutumika kwa ajili ya kukinga maradhi ya kichocho , matende na minyoo

Tangu kuanza zoezi la utoaji wa madawa za kinyoo , matende na minyoo matatizo hayo yamepungua kwa wananchi kisiwani na pemba na kushauri wananchi kutoa taarifa kwa maafisa wa afya baada ya kupata matatizo baada ya kuzitumia dawa hizo .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.