Habari za Punde

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) Yatiliana Saini ya Makabidhiano ya Jengo la Nyumba ya Treni Darajani kwa Kampuni ya CRJE Kwa Ajili ya Ujenzi Wake.

Ujenzi wa Jumba la Treni Zanzibar kuaza muda wowote kuazia sasa baada ya makubaliano ya kwanza kukabidhia mjenzi wa jumba hilo kwa kampuni ya Ujenzi ya China ya CRJE baada ya kutiliana saini ya makabidhiano ya jengo hilo kwa pande hizo mbili kati ya ZSSF na CRJE. makubaliano hayo yamefanyika katika viwanja vya jumba hilo darajani Zanzibar.
Meneja Mipango na Uwekezaji wa ZSSF Ndg Khalifa Muumin, akizungumza na Wajenzi wa Jengo la Nyumba ya Treni Darajani kabla ya kuaza kwa hafla ya utilianaji wa saini ya makabidhiano ya jengo hilo kwa Mkandarasi Kampuni ya Kichina ya CRJE, akimsikiliza Meneja Mkaazi wa Kampuni hiyo ya CRJE Mr. Bai Hao Chen. akisisitiza jambo wakati wa mazuyngumzo hayo. 
Wataalamu wa Kampuni ya CRJE wakiwa katika viwanja vya jengo hilo wakisubiri kutiliana saini ya makabidhiano ya jengo hilo ikiwa hatua ya mwanzo kwa ajili ya kuaza ujenzi wake kujenga maduka ya kisasa. 
Msimamizi Ujenzi huo wa jengo la Treni Darajani wa Kampuni ya Cons African Ltd . Eng Francis D Kaloko akitowa maelezo ya utaratibu wa ujenzi huo kwa pande hizo mbili za ZSSF na CRJE, kabla ya utilianaji wa saini hiyo ya kukabidhiwa jengo hilo kwa mkandarasi.
Msanifu Majengo wa Kampuni ya Cons African Ltd Moleka , akitowa maelezo kabla ya kuaza kwa utilianaji wa saini ya makabidhiano ya jengo hilo kuaza ujenzi wake unaotarajiwa kujengwa na Kampuni ya Kichina ya CRJE. 
Meneja Mkaazi wa Kampuni ya Ujenzi ya Kichina ya CRJE Bai Hao Chen, akimsikiliza Msimamizi wa Ujenzi huo Eng. Francis D Kaliko, akitowa maelezo ya utaratibu wa ujenzi huo wa Jengo la Nyumba ya Treni Darajani Zanzibar. 
Zoezi la utilianaji wa saini ya makabidhiano ya Jengo la Darajani Jumba la Treni kwa kampuni ya Kichina ya CRJE kwa ajili ya kuaza kwa ujenzi huo. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) Abdulwkil Haji Hafidh akibanilishana mkataba wa makabidhiano ya jengo la Jumba la Treni Daraji, Meneja Mkaazi wa Kampuni ya CRJE Bai Hao Chen baada ya kuliliana saini ya makabidhiano hayo kwa hatua za mwanzo kuaza ujenzi wake.
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.