Habari za Punde

Mkutano wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Ukiendelea Katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar

Wajumbe wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki kushoto Mhe Suzan Nakawuki na Mhe Margret Zziwa wakiwa nje ya ujumbe wa mkutano kabla ya kuaza Mkutano huo wakibadilishana mawazo. 
Waheshimiwa Wabunge wakiwa katika ukumbi wa mkutano wakibadilishana mawazo kabla ya kuaaza kwa Bunge hilo leo jioni. 
Wakifurahia jambo wakati wakibadilisha mawazo kabla ya kuaza kwa Bunge hilo.
Mjumbe wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhe Abdallah Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na mwandishi wa habari wa gazeti la Habari leo wakati akiwasili katika ukumbi wa mkutano kuhudhuria Bunge hilo.

Wajumbe wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika Ukumbi wa Mkutano wakihudhuria Mkutano huo.
Mhe Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhe Daniel F Kidega akiongoza Bunge hilo linalofanyika katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar. akizungumza kabla ya kuwasilishwa kwa Ripoti hiyo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo Utalii na Maliasili. 
Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo Utalii na Maliasili Mhe Patricia M Hajabakiga akiwasilisha ripoti hiyo katika Mkutano wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki.Wajumbe wakipitia ripoti ya Kamati ya Kilimo Utalii na Maliasili wakafuatilia wakati ikiwasilishwa katika Mkutano huo wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Masharki. linalofanya mkutano wake Zanzibar kwa mara ya pili mkutano wa kwanza umefanyika mwaka 2007.
Wajumbe wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki wakifuatilia ripoti ya Kamati ya Kilimo Utalii na Maliasili inayowasilishwa ma Mjumbe wa Kamati hiyo Mhe Patricia Hajabakiga kutoka Rwanda  hayupo pichani.
Mjumbe wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Kenya Mhe, Peter Mathoki akichangia ripoti hiyo
Mbunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Tanzania Mhe Shyrose Bhanji akichangia Ripoti ya Kilimo Utalii na Maliasili iliowasilishwa katika Mkutano huo wa Bunge la Afrika Mashariki katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.  
Mbunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mahariki kutoka Zamzibar Mhe Maryam Ussi Yahya akichangia wakati wa mkutano huo wa Bunge, katika ukumbi wa baraza la Wawakilihi Chukwani Zanzibar.
Mheshimiwa Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhe Daniel F Kidega, akiongoza Mkutano wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar. 
Waheshimiwa wakiwa makini kufuatilia michango ya Wajumbe wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalofanyika Zanzibar katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar.
Mjumbe wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Tanzania Mhe. Twaha Issa Taslima akichangia ripoti hiyo iliowasilishwa.
Waheshimiwa wakifuatilia michango wa Wajumbe wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhe Makongoro Nyerere akiwa makini kusikiliza michango hiyo ikiwasilishwa.
Mbunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Tanzania Mhe Abdallah Ali Hassan Mwinyi akichangia katika mkutano huo wa Bunge la Afrika Mashariki mkutano wake unaofanyika Zanzibar.  
Mbunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Uganda Mhe. Mike Sebala akichangia ripoti hiyo baada ya kuwasilishwa katika Bunge hilo na kujadiliwa.
Waheshimia Mawaziri wa Nchi za Afrika Mashariki wakifuatilia michango ya ya Wabunge wakichangia Ripoti ya Kilimo Utalii na Maliasili.iliowakilisha katika Mkutano huo wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki mkutano wake unaofanyika Zanzibar katika Jengo la Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar.
Wagenin waalikwa kutoka sekta ya Kilimo Zanzibar wakifuatilia Bunge hilo likizungumzia Kilimo, Utalii na Maliasili katika Afrika Mashariki. wakiwa katika sehemu ya wageni katika ukumbi huo.wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.