Habari za Punde

Wananchi walalamika kituo cha Polisi kufungwa usiku na kunywa pombe

Na Mwandishi wetu, Pemba

Wananchi wa shehia ya Kengeja wilaya ya mkoani mkoa wa kusini Pemba  wamelililamikia jeshi la Polisi nchini kwa kituo cha Kengeja kukifunga ifikapo usiku na baadhi ya askari kituoni hapo wakijishusisha na vitendo viovu vya ulevi hali ambayo inawapelekea kusumbuka pindi wanataka msaada kituoni hapo.

Wamesema kua,tatizo hilo ni la muda mrefu sasa na kila siku hali inavyokwenda ndivyo hali inavyokua mbaya kituoni hapo.

Hayo yameelezwa  na baadhi ya wanachi wa maeneo hayo kwa nyakati tofauti walipokua wakizungumza na mwandhishi wa habari hizi aliyefika kijijini huko kufuatia malalamiko juu ya kadhia hiyo.

Mmoja miongoni mwa wanakijiji hicho ambae hakupenda jina lake lidhihirishwe amesema kua,hali ni mbaya katika kituo hicho amesema inapofika majira ya saa nne usiku muda wowote kituo hicho kinafungwa na huduma kutopatikana tena kuanzia muda huo mpaka asubuhi.

“kwakazi zangu, mara nyingi huwa narudi nyumbani usiku, nikipita kituo kimefungwa sasa najiuliza kama napatwa na tatizo usiku huo kimbilio langu ni pale kituoni lakini kinafungwa sasa nitafanya nini”alisema mkaazi huyo.

Akizungumzia suala la ulevi kwa askari wa kituo hicho amesema kua, ni aibu kwa kituo hicho ingawa si wote lakini wapo baadhi yao hulewa mpaka muda wakazi.

Amesema inafika wakati mtu anakwenda mapokezi kupeleka maelezo ya jambo Fulani lakini anapigwa na mshangao kwa jinsi anaekupokea na kuandika shida yako akiwa hoi kwa ulevi.

Sheha wa shehia hiyo Ndg: Muhammed Kassim Afrika alipoulizwa na mwandhishi wa habari hizi juu ya kadhi hizo kwa askari wa kituo hicho amethibitisha na kukubali wazi uwepo wa askari walevi na kituo hicho kufungwa nyakati za usiku.

Amesema kuanzia muda wa saa nne au saa sita usiku kituo hicho kinafungwa na baadhi ya wananchi hukosa humuda kituoni hapo.
Akizungumza kwa hamasa sheha huyo ameungana na wananchi kwa kusema kua kadhia hiyo ni ya muda mrefu na ameshawahi kufikisha kilio hicho kwa kamanda wa polisi mkoa lakini mpaka leo hali bado haijarekebishika.

Akigusia suala la askari wa kituo hicho kulewa wakati wa kazi amethibitisha madai hayo  huku akitilia mkazo sula hilo “ingawa sio wote lakini wapo baadhi yao wanalewa haswa tena kulewa”alisema sheha huyo.

Kufuatia madai hayo ya wananchi yaliyotiliwa mkazo na sheha wa shehia hiyo mwandishi  wa habari hizi alikwenda mpaka katika afisi za kamanda mkoa wa kusini Pemba  Jeshi la polisi kituo cha Polisi Madungu na kuzungumza na kamanda huyo Sekhan Muhammed Shekhan.

Akijibu suala la mwandishi wa habari aliyetaka kujua juu ya askari  wa kituo hicho kulewa Shekhan amesema,jambo hilo ameshalitolea taarifa kwa mwandishi wa habari wa awali aliyetaka kujua juu ya kadhia hiyohiyo kua kuna matatizo kidogo katika maeneo ya kituo hicho.

Amesema sio  askari wote wanaolewa  ila ni mmoja tu na hatua zimeshaanza kuchukuliwa kwa askari huyo.

Akitaja hatua hizo walizozichukua dhidi ya askari huyo amesema,wamemuweka karibu na kamati zao za maadili ili kumchunguza zaidi na watakapomuona anaendelea na vitendo hivyo watamchukulia hatua za kumfukuza kazi na mpaka sasa wameshamuandikia barua ya tahadhari.

Katika suala la kufungwa a kituo hicho nyakati za usiku amesema jambo hilo pia amelisikia na  bado wanaendelea kuchunguza kwa kamini kwani sio suala la kuliharakisha.

 “sisi tuna maafisa  mabalimbali amabao tumewapanga sehemu tofauti kwa kuchugunguza mambo kama hayo na baada ya kupata taarifa rasmi totatoa  jibu na ikibainika kinafungwa kweli tutamwita mkuu wa kituo kueleza ni sheria gani iliyompa kufunga kituo hicho  ambacho ni class “A”kwa sababu vituo kama hivyo havitakia kufungwa  ila vinatakiwa kutoa humuda muda wote” alisema Kamanda Shekhan.

Amemalizia kwa kusema kua mpaka muda huu bado hawajawahi kuona kituo hicho kufungwa amesema labda kilifungwa kwa bahati mabaya

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.