BIKOMBO Madina Hamad wa shehia ya Mjini Ole
wilaya Chakechake, ambae amefanikiwa kubakia ndani ya nyumba aliokuwa ameolewa
na kuachwa na watoto nane, baada ya kusaidiwa na mradi wa GEWE-TAMWA, ambapo
kwa sasa ameanzisha kilimo cha mboga mboga na kujikimu walau kwa chakula, huku
akiwa pia kwenye mpango wa kunusuru kaya masini kupitia TASAF III, wakati akizungumza
na mwandishi wa habari Haji Nassor, (Picha
na Fatma Hamad, Pemba).
WARATIBU wa wanawake na watoto pamoja na wasaidizi wao wa
shehia za Kinyikani, Kiungoni, Mjini ole, Kangagani, Mchanga mdogo na Shengejuu
wakiwa katika picha ya pamoja, baada ya kumalizika kwa mradi wa GEWE –TAMWA ndani ya shehia zao, halfa hiyo ilifanyika
Tibirinzi Chakechake, (Picha na Haji
Nassor, Pemba).
MRATIBU wa wanawake na watoto shehia ya
Mjini Ole, Khadin Nenock Maziku, akizungumza na mwandishi wa habari wa shirika
la magazeti ya serikali Zanzibar ofisi ya Pemba Haji Nassor, juu mafanikio ya
mradi wa GEWE -TAMWA, ambao unamalizika mwezi Disemba mwaka huu (Picha na Fatma Hamad, Pemba).
SHEHA wa shehia ya Mchanga mdogo Assa
Makame Said, akitoa ufafanuzi wa namna ya kupambana na matendo ya
udhalilishaji, kwenye hafla ya kufungwa kwa mradi wa GEWE-TAMWA iliofanyika Kiuyu
Kigongoni wilaya ya Wete Pemba, (Picha
na Haji Nassor, Pemba).
WARATIBU wa wanawake na watoto pamoja na masheha wa
shehia sita za wilaya ya Wete, zilizokuwemo ndani ya mradi wa GEWE, wakiwa
kwenye hafla ya kufungwa kwa mradi huo, iliofanyika Kiuyu Kigongoni wilaya ya
Wete Pemba, (Picha na Haji Nassor,
Pemba).
SHEHA wa shehia Kiungoni wilaya ya Wete
Pemba, Omar Khamis Othman, akizungumza kwenye hafla ya kufungwa mradi wa GEWE,
uliokuwa ukiendeshwa na TAMWA, hafla hiyo ilifanyika Kiuyu Kigongoni wilayani
humo, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
No comments:
Post a Comment