Habari za Punde

Waziri Amina akutana na wazalishaji chumvi kisiwani Pemba

 
Kufuatia Tanzania kuelekea kua nchi ya viwanda na hatimae Zanzibar nayo ipo mbioni na hatua mbalimbali zimeanza kutekelezwa ili kufikia huko ifikapo 2020. 

Mh Waziri wa biashara , viwanda na masoko Zanzibar Amina Salum Ali jana alikua na maongezi maalum baina yake na wazalishaji chumvi kisiwani Pemba ambapo kwa namna moja ama nyengineyo nao ni wadau miongoni mwa wataokaofanikisha kuifikisha Zanzibar huko. 

Pia waziri huyo alikua na ziara maalum ya kuwatembelea wakulima wa mbogomboga na wakulima wa mazao ya karafuu pamoja na viungo vyengine mbalimbali,ambapo katika ziara hiyo alitoa miongozo kwa walima hao ili kufanikisha uzalishaji bora na upatikanaji wa soko la uhakika. 

 Sikiliza mahojiano maalum baina ya waziri huyo na mwandishi wa habari Salmin Juma aliyetaka kujua ni kwa kiwango gani Zanzibar inakwenda kufanikiwa kua nchi ya viwanda ifikapo 2020.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.