Habari za Punde

Mafunzo ya kukabiliana na maafa kwa shehia hizo zilizoko katika visiwa Vidogo vidogo Pemba



 MKUU wa Wilaya ya Mkoani Mhe:Hemed Suleiman Abdalla, akifungua mafunzo ya siku moja ya kukabiliana na maafa, kwa sheria tatu zilizokatika visiwa vidogo vidogo huko Wilaya ya Mkoani.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 AFISA kutoka kamisheni ya kukabiliana na maafa Pemba, Ali Salum Ali akiwasilisha mada kwa wajumbe wa kamati za kukabiliana na maafa kutoka shehia tatu zilizoko katika Visiwa Vidogo Vidogo Wilaya ya Mkoani.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 MMOJA wa wajumbe wa kamati ya kukabiliana na maafa kutoka shehia ya Kisiwa Panza, akichangia katika mafunzo ya kukabiliana na maafa yaliyotolewa na Kamisheni ya kukabialiana maafa Pemba, huko katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mkoani.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 AFISA kutoka Kamisheni ya Kukabiliana na maafa Pemba, Mbela Issa Mbela akiwasilisha mada katika mafunzo ya kukabiliana na maafa kwa shehia tatu zilizoko katika Visiwa vidogo vidogo.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 WANANCHI kutoka shehia tatu shehia ya Makoonge, Shehia ya Kisiwa Panza na shehia ya Mwambe Shamiani, wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Mhe;Hemed Suleiman Abdalla, wakati alipokuwa akifungua mafunzo ya kukabiliana na maafa kwa shehia hizo zilizoko katika visiwa Vidogo vidogo Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
Dk Suleiman Mohamed Ali kutoka Red Cross Kisiwani Pemba, akionyesha mmfano wa kumsaidia baada ya kupatwa na maafa ya kuungua moto mkono kwa kuutumbukiza mkono huo katika maji yaliyobari, wakati wa utoaji wa mafunzo ya kukabiliana na maafa kwa shehia tatu za Wilaya ya Mkoani zilizoko katika Visiwa Vidogo Vidogo.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.