Habari za Punde

Mashabiki wa Timu ya Yanga Afrika Zanzibar Wakipanga Mkakati Timu Yao Kulitowa Kombe la Mapinduzi 2017.

Akitoa taarifa kwa mwandishi wa blog hii shabiki wa timu hiyo dokta Cosmass alisema asubuhi ya leo walifanya kikao kwa ajili ya kujadili ujio wa timu yao.
"Tumekubaliana kuipokea timu kwa beni pale bandarini siku ya Jumamosi itakapowasili".

Alisema mipango mingi imepangwa kuhakikisha Yanga wanatwaa ubingwa wa mashindano hayo yanayoingia mwaka wa 11 tangu kutambulika rasmi.
Aidha Cosmass amedai kuwa kikao hicho kimekubaliana kuomba dua kwa kila mtu na imani yake ili timu yao ifike fainali na wakutane na Simba kwenye Simba la Amaan.

Yanga imepangwa kundi B la mashinfano hayo ikiwa pamoja na timu za Azam, Zimamoto na Jamhuri kutoka Pemba.

Mara ya mwisho kwa Yanga kufika fainali za kombe la mapinduzi ilikua mwaka 2011 ambapo ilifungwa bao 2-0 na hasimu wake Simba huku ikinyakua ubingwa wa michuano hiyo mwaka 2007 ilipovheza na Mtibwa Sugar.

Mashindano ya kombe la mapinduzi yanatarajiwa kuanza rasmi hapo kesho majira ya saa mbili na robo usiku kwa mchezo mkali kati ya timu zenye upinzani visiwani Zanzibar, Taifa ya Jang'ombe watakaocheza na Jang'ombe Boys.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.