Habari za Punde

Timu ya Jamuhuri Kuifuata Yanga Jumamosi Kombe la Mapinduzi Zanzibar.

Kikosi cha wachezaji 22 na viongozi tisa wa timu ya Jamhuri kutoka kisiwani Pemba kinatarajiwa kuwasili Unguja Jumamosi ya wiki hii kwa ajili ya mashindano ya kombe la Mapinduzi.

Akitoa taarifa kwa Blog hii meneja wa Jamhuri Abdalla Abeid 'Elisha' alisema kikosi hicho kinakuja kwenye mashindano hayo huku wakiwa na shauku ya kuunyakua ubingwa.

"Wachezaji walimhakikishia kocha kuwa wanataka kuwatoa kimasomaso Wazanzibar kwa kulikosa kombe hili muda mrefu"

Jamhuri ambayo kwa sasa inafundishwa na kocha Abdulmutik Kiduu iliwahi kutinga fainali za mashindano hayo mwaka 2012 na kufungwa bao 3-1 na Azam kwenye pambano hilo.

Kikosi hicho kilichopangwa kundi B na Yanga, Azam na wenzao wa Zimamoto kitaanza kushuka dimbani Amaan Jumatatu ya Januari 2, saa mbili na robo usiku kupepetana na Yanga.

Mara ya mwisho kwa timu ya Zanzibar kuchukua ubingwa ilikuwa mwaka 2009 kwa Miembeni kuifunga KMKM kwenye dimba la Gombani kisiwani Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.