Habari za Punde

Shaka Hamdu Azindua Rasmin Kampeni ya Jogging UVCCM Mkoani Kagera.

Kaimu katibu mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka (Mnec)  wa tatu kulia akiongoza zoezi la jogging wilaya karagwe pamoja na Viongozi Mbali mbali wa chama na Serikali 
Kaimu katibu mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka wa katikati akiendeleza zoezi la jogging pamoja na Mwenyekiti wa UVCCM  Wa Uvccm Mkoa wa Karagwe Ndg Yahaya Kateme wa kwanza kushoto.
Kaimu katibu Mkuu Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi Taifa Shaka Hamdu Shaka akiruka Mchaka mchaka katika viwanja vya CCM Wilaya ya karangwe
Kaimu katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka wa pili kulia akiendelea na Zoezi la Unyooshaji wa Viungo pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Mhe. Godfrey Ayub  Mheluka
Katibu UVCCM Mkoa wa Kagera Ndg:Didas Zimbile akiongoza Zoezi la Unyooshaji wa Viungo katika Viwanja vya CCM Wilaya ya Karagwe mapema.
Kijasho chembamba kikimtiririka Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kagera Ndg:Yahya Kamteme katika zoezi la unyooshaji wa Viungo Vya Mwili katika Viwanja Vya CCM Wilaya ya Karagwe.

Kaimu katibu Idara ya Hamasa,Sera,Utafiti na Mawasiliano Ndg Mtemi Slyvester Yaredi akiendelea na zoezi la kunyoosha viungo 

Na Mwandisgi Wetu.

Kaimu katibu mkuu Uvccm Taifa ndg Shaka H.Shaka leo amezindua rasmi kampeni ya Jogging UVCCM yenye kauli mbiu ya 'MAZOEZI KWA AFYA' iliyozinduliwa Kitaifa Wilayani Karagwe.

Katika Mazozi hayo Kaimu katibu mkuu ameshiriki jogging na Mazoezi Viungo akiongozwa na Mwenyekiti  Uvccm mkoa wa Kagera ndg YAHYA KATEME,Mkuu wa Wilaya Karagwe  Mhe. Godfrey Ayub  Mheluka pamoja na vijana na viongozi mbalimbali  Wa Chama na Serikali Wilayani humo.  

Akiongea  mara baada ya Mazoezi hayo Ndg: kaimu katibu mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka amewataka Makatibu wa UVCCM Ngazi za Wilaya Nchini kote kuzingatia maelekezo yaliyotolewa tangu Mnamo tarehe 24 Mwezi Oktoba 2016 la kuanzisha jogging Club alisema "nitumie fursa hii kuwapongeza sana kwa kutambua umuhimu wa mazoezi, sasa Vijana lazima wawe wakakamavu na tayari muda wote hatuwezi kuwa na taifa la vijana goigoi wasio jiweza kama ambavyo  hata makamu wa Rais alivyounga mkono katika swala hili la mazoezi " Pia amewataka vijana wote kushiriki ipasavyo Zoezi hili amesema '' Jogging ni swala muhimu sana kwa vijana kwani pamoja na kujenga miili yetu jogging itatufanya tuwe wamoja t wenye ushirikiano wa kudumu haswa katika mambo mbali mbali ya kijamii''.

 Kaimu katibu mkuu yupo katika ziara ya siku nane mkoani Kagera ambapo atatembelea wilaya zote 8 za mkoa wa Kagera.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.