STATE
HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF
THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Dar-es-Salaam 16.12.2016

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.
Ali Mohamed Shein, amewaongoza viongozi, wakuu wa vikosi vya Ulinzi na Usalama
pamoja na wanafamilia kuuaga mwili wa Marehemu Bregedia Jenerali Cyril Ivor
Mhaiki, Kamanda wa Brigedia ya Nyuki Zanzibar,aliyefariki dunia tarehe 13,
Disemba 2016 katika Hospitali ya Jeshi la Wananchi wa Tanzaia, Lugalo Dar-es-Salaam.
Mwili wa Marehemu
Brigedia Jenerali Cyril Ivor Mhaiki umeagwa leo huko katika Hospitali ya Jeshi
la Wananachi wa Tanzania, Lugalo jijini Dar-es-Salaam ambapo Dk. Shein alifika Hospitalini
hapo, majira ya saa nne za asubuhi akitokea Zanzibar akiwa ameongozana na
viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiwemo Mawaziri na
Watendaji wengine wa Serikali.
Akiwa Lugalo Dk. Shein
alipokewa na viongozi mbali mbali wakiongozwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussen Mwinyi,
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Davis Adolf Mwamunyange, viongozi
wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Viongozi wengine wakuu wa
vikosi vya Ulinzi na Usalama ambapo Dk. Shein aliaanza kwa kutia saini kitabu
cha maombolezo.
Katika tukio hilo ambapo
baadhi viongozi wakuu wa Jeshi wastaafu walihudhuria, Dk. Shein aliongoza
waombolezaji kutoa salamu za mwisho, ambapo salamu mbali mbali zilitolewa
kutoka kwa viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania pamoja na makundi maalum.
Katika salamu za rambi
rambi zilizotolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekitiwa Baraza la Mapinduzi
ambazo zilisomwa na Bregedia Jenerali
Kayombo zilieleza namna Dk. Shein, pamoja na wananchi wote wa Zanzibar
walivyopokea kwa mshtuko taarifa ya kifo cha Kamanda huyo hodari, aliyetoa
mchango mkubwa katika shughuli za ulinzi na usalama na maendeleo ya Tanzania
kwa jumla.
Salamu hizo zilieleza
namna Marehemu Mhaiki alivyokuwa mtu mwenye mashirikiano na wenziwe, muadilifu,
msikivu na Kamanda mahiri katika kazi zake.
Salamu nyengine mbali
mbali za rambi rambi zilitolewa zikiwemo salamu kutoka Baraza la Michezo ya
Majeshi Tanzania (BAMATA) ambalo
Marehemu alikuwa Mwenyekiti wa Baraza hilo, salamu ambazo zilieleza namna
alivyokuwa mstari wa mbele katika kuimarisha na kuiendeleza michezo ya Majeshi
na hatimae kupata mafanikio makubwa ndani na nje ya nchi.
Aidha, salamu hizo
zilieleza kuwa Jenerali Mhaiki atakubukwa katika mchakato wa kurejesha
mashindano katika kikosi hicho na tangu kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa BAMATA
mnamo Septemba, 24 mwaka 2013 mafanikio makubwa yameweza kupatikana na kuahidi
kuyafuata mazuri yote aliyoyaacha.
Akitoa neno la
shukurani kaka wa Marehemu Oliva Mhaiki, alimsukuru Rais wa Zanzibar nan
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk.Ali Mohamed Shein kwa kwenda kuungana nao
katika kuuaga mwili wa mdogo wake pamoja na viongozi wote aliohudhuria katika
tukio hilo.
Brigedi ya Nyuki
Zanzibar nayo ilitoa salamu zake za rambi rambi kwa kifo cha Bregedia wake
Jenerali Cyril Ivor Mhaiki na kusisitiza kuwa ameacha pengo kubwa kwa Brigedi
hiyo, familia pamoja na Jeshi la Wananchi wa Tanzania na nchi kwa jumla
sambamba na kukumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika malezi ya askari.
Kaka huyo wa Marehemu
alitumia fursa hiyo kutoa shukurani kwa madaktari wa hospitali hapo kwa
kumuuguza marehemu pamoja na kutoa shukurani kwa Jeshi la Ulinzi Tanzania kwa
kutoa huduma kwa ndugu yake.
Mwili wa marehemu
umesafirishwa leo kutoka Hospitalini hapo kuelekea Songea Mkoani Ruvuma ambako mazishi ya
Jenerali Mhaiki yatafanyika siku ya Jumaapili Disemba 18, mwaka huu sambamba na taratibu
zote za kijeshi, ambapo pia, salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.
Johm Pombe Magufuli zitatolewa katika mazishi hayo.
Marehemu Mhaiki
amezaliwa Disemba 16 mwaka 1954 huko Mbinga Ruvuma na kupata elimu ya Msingi na
Sekondari katika skuli na vyuo tofauti ambapo alijiunga na Jeshi mnamo mwaka
1973 na kupata Kamisheni mwaka uliofuata na kupita ngazi tofauti na hatimae kupandishwa
vyeo na kufikia Bregedia Jenerali hadi kufariki kwake.
Sambamba na hayo,
Jenerali Mhaiki alitunukiwa medali mbali mbali kutokana na uongozi wake mahiri.
Marehemu Mhaiki ameacha Mjane na mtoto mmoja.
Rajab Mkasaba, Ikulu
Zanzibar
Postal Address: 2422
Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment