Habari za Punde

Wanafunzi 3815 waendelea na masomo elimu ya watu wazima kisiwani Pemba

Na Salmin Juma, Pemba

JUMLA ya wanafunzi  3815 waliokosa elimu ya lazima wamejiunga na  madarasa ya kisomo cha elimu ya watu wazima na  wanaendelea na masomo katika  madarasa hayo kutoka Wilaya zote nne  za Kisiwa cha Pemba , huku wengi wao ni wanawake .

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya Mitihani ya upimaji wa wanakisomo , Maratibu wa Idara ya Elimu Mbadala na watu wazima Pemba Hija Hamad Issa amesema kuwa kati ya wanafunzi hayo  wanawake ni 3325 na wanaume ni 490.

Ameeleza kwamba  wanafunzi hao wanaendelea na masomo yao hatua  tofauti ambapo wapo walioko hatua ya kwanza , wengine ya pili ,  , hatua ya tatu na nne na wanaendelea na mitihani ya upimaji inayofanyika Unguja na Pemba .

Aidha amezidi kufafanua kwamba  Wilaya ya Mkoani  ndiyo inayoongoza kwa kuwa na wanakisomo wengi ukilinganisha na Wilaya nyengine za Pemba ikiwa na wanakisomo 1218 wanawake ni 1006 na wanaume ni 212.

Ikifuatiwa na Wilaya ya  Wete  yenye wanakisomo 1146 , wanawake 1029 na wanaume ni 117 , Wilaya ya Micheweni nayo ikiwa na wanakisomo 908 , wanawake ni 820 na wanaume ni 88.

Kwa mujibu wa mratibu huyo ni kuwa Wilaya ya Chake Chake ina jumla ya wanakisomo 543 ambapo wanawake ni 470 na wanaume ni 73.

“Tunao wanafunzi 3815 wa kisomo cha elimu ya watu wazima Kisiwani Pemba huku idadi kubwa ni wanawake ambao wanafikia 3325,  maendeleo yao yanaonyesha mafanikio ya kwamba wameondokana na suala la kutojua kusoma , kuandika na kuhesabu ”alisema .

Hata hivyo idadi hiyo inaweza kuongezeka iwapo Idara itafanikiwa kuondoa changamoto za ukosefu wa miwani , kwani baadhi ya wanakisomo wanashindwa kuhudhuria kutokana na kukabiliwa na changamoto ya uoni hafifu.

Akitoa ufafanuzi juu ya suala hilo , Mkurugenzi wa Idara ya Elimu Mbadala na Watu Wazima Mashavu Ahmad Fakih ameiomba Wizara ya elimu na Mafunzo ya amali kuweka fungu kwa ajili ya kusaidia kuzitatua changamoto hiyo ili kuongeza idadi ya wanakisomo .

“Wakati Serikali inaendelea kutafuta ufumbuzi wa changamoto hizo , ni vyema wanakisomo wenye wakajitolea kununua miwani katika vituo vya afya na hospitali ”alishauri Mashavu .

Aidha Mkurugenzi huyo aliwataka pia wahusani , mashirika na viongozi wa Majimbo kushirikiana na Idara kusaidia baadhi ya changamoto zinazoyakabilia madarasa ya kisomo ikiwemo suala la vifaa vya kusomea  vikalio na majengo .

Hata hivyo ,Mashavu amepongeza juhudi zinazochukuliwa na akinamama kwa kujiunga na madarasa hayo ambayo yemelenga kuwa komboa kutoka katika wingu zito la kutojua kusoma , kuandika na kuhesabu .

Wanakisomo hao pia wameshauriwa kuviimarisha vikundi vyao ya kuweka na kukopa  pamoja na vikundi vya ujasiriamli ambavyo wamevianzisha kwa lengo la kujikomboa na hali ya umaskini wa kipato 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.