Habari za Punde

Kaimu Katibu Mkuu UVCCM aanza ziara mkoa wa Kagera

 Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka (MNEC) Akiwasili na Kulakiwa na Viongozi Wa Chama na Serikali Mkoani Kagera katika kijiji cha Kahina Mpakani mwa Mkoa wa Geita nA Kagera
 Mhe:Mkuu Wa Wilaya ya Biharamulo Bi Saada Malinde akimkabidhi Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka (MNEC) Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)katika kikao cha ndani 
 Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka (MNEC akielekea kukutana na Wana CCM Wilayani Biharamulo 
 Mwenyekiti Wa UVCCM Yahya akizungumza  katika mkutano wa Diwani wa kata ya NEMBE na Wananchi 
 Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka (MNEC) Pamoja na mhe: DIWANI wa kwanza Kushoto akigawa kadi 115 Kwa wanachama Wa CCM UVCCM na WAZAZI Pia ameweza kukaribisha wanacha toka Chama cha CDM 30 
 Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka (MNEC Akinywa Maji mara Baada ya kukagua Mradi wa Maji katika kata ya NYANTANGARA
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka (MNEC)akizindua Ofisi ya Chama kata ya KABINDI Lililo gharimu shilingi Million 3


Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka  (MNEC) Leo umeanza ziara ya siku 8  katika mkoa wa Kagera ambapo atatembelea  wilaya zote 8 za mkoa huo.

Katika wilaya ya Biharamulo Leo Kaimu Katibu Mkuu alifanya shughuli mbali mbali za kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM 2015-2020 pamoja na kufanya shughuli za kuimarisha chama na jumuiya zake kama:

Alipokea taarifa ya wilaya ya Biharamulo kuhusu utekelezaji wa  kazi za Chama, jumuiya ya UVCCM na Serikali.

Alishiriki ujenzi wa nyumba ya maabara na walimu katika kijiji cha  Kaniha.

Alikagua mradi wa maji safi na salama na uchimbaji wa visima vya maji katika kijiji cha Nyantakaro

Alipata fursa ya kuzungumza na vijana na wananchi wa ujumla katika kijiji cha Nemba na kusikiliza kero, changamoto na maoni ya vijana na  wananchi hao.

Alishiriki na kufungua wa jengo la kisasa la ofisi ya CCM kata ya Kabindi.

Alikabidhi kadi 115  za CCM, vijana, wazazi na amekabidhi kadi 30 kwa wanachama wapya kutoka CHADEMA waliojiunga na CCM

Katika ziara hiyo amefuatana na viongozi kadhaa wa  Serikali Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo Sasa Malunde, Mkurugenzi wa Halmashauri na maafisa waandamizi wa kada mbali mbali serikalini ambao walitakiwa kujibu mambo kadhaa yaliyokuwa yakijitokeza yanahusiana na utekelezaji wa ilani ya CCM na maendeleo kwa ujumla.

Wengine ni viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na jumuiya zake ambapo kesho  ziara hiyo itaendelea wilaya ya Ngara.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.