Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Mwinyi Amejumuika na Wananchi katika Maziko ya Marehemu Zulekha Ahmed Abdalla

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa  Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussei Ali Mwinyi  akijumuika na Viongozi wa Serikali, Dini na Wananchi katika Sala ya  Maiti, aliyekuwa Mke wa Marehemu Sheikh.Hyder Jabir Saleh E-Farsy,Marehemu  Zulekha Ahmed Abdallah, ikiongozwa na Mtoto wa  Marehemu Sheikh Ahmad Hyder Jabir E-Farsy,iliyofanyika katika Msikiti wa Mkuu wa Ijumaa Malindi Wilaya Mjini Unguja Jijini Zanzibar, na (kulia kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Alhajj Othman Masoud Othman na (kushoto kwa Rais) Mbunge wa Jimbo la Mahonda Mhe. Abdalla Hassan Mwinyi na Mtoto wa Marehemu Sheikh Kassim Hyder Jabir
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa  Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussei Ali Mwinyi  akijumuika na Viongozi wa Serikali, Dini na Wananchi katika kuitikia dua ya kumuombea Marehemu Zulekha Ahmed Abdallah, baada ya kumalizika kwa Sala ya Maiti,iliyofanyika katika Msikiti wa Mkuu wa Ijumaa Malindi Wilaya Mjini Unguja Jijini Zanzibar, na (kulia kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Alhajj Othman Masoud Othman na (kushoto kwa Rais) Mbunge wa Jimbo la Mahonda Mhe. Abdalla Hassan Mwinyi na Mtoto wa Marehemu Sheikh Kassim Hyder Jabir


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa  Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussei Ali Mwinyi  akijumuika na Viongozi wa Serikali, Dini na Wananchi katika maziko ya aliyekuwa Mke wa Marehemu Sheikh.Hyder Jabir Saleh E-Farsy,Marehemu Zulekha Ahmed Abdallah,yaliyofanyika katika viwanja vya Msikiti Mkuu wa Ijumaa Malindi Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi akiweka mchanga katika kaburi la Marehemu Zulekha Ahmed Abdalla, aliyekuwa Mke wa Marehemu Sheikh Hyder Jabir Saleh E-Farsy, wakati wa maziko hayo yaliyofanyika katika viwanja vya makaburi ya Msikiti wa Ijumaa Malindi Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Wananchi na Masheikh katika kuitikia dua ya kumuombea aliyekuwa Mke wa Marehemu Sheikh. Hyder Jabir Saleh E-Farsy. Marehemu Zulekha Ahmed Abdalla, baada ya kumalizika kwa maziko hayo yaliyofanyika katika makaburi ya Msikiti wa Ijumaa Malindi Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar, na (kulia kwa Rais ) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na (kushoto kwa Rais) Mjukuu wa Marehemu Khalil Kassim Hyder
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsalimia na kutowa mkono wa pole kwa Mtoto wa Sheikh Ahmad Hyder Jabir E-Farsy, baada ya kumalizika kwa maziko ya Marehemu Zulekha Ahmed Abdalla, yaliyofanyika katika makaburi ya Msikiti wa Ijumaa Malindi Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.