Habari za Punde

Balozi Seif ashiriki katika maulidi ya Mtume ( SAW) yaliyoadndaliwa na Uongozi wa Msikiti wa Ijumaa wa Majmuati Islamia Temeke


 Viongozi wa Kitaifa wakijumuika pamoja na Waumini wa Dini ya Kiislamu kwenye Mlango wa Nne wa Barzanji wenye kisimamo cha kumtukuza Mtume Muhammad {SAW}.
 Baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislamu wakiendelea na hafla ya Maulidi ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad {saw} hapo Temeke Jijini Dar es salaam

Waislamu wakiwa makini kusikiliza mawaidha na nasaha zilizokuwa zikitolewa na Viongozi wa Dini ya Kiislamu katika Hafla ya Maulidi ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad {SAW} hapo Temeke Jijini Dar es salaam.
 Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir Ali akitoa darsa kwa Maelfu ya Waumini wa Dini ya Kiislamu waliohudhuria Maulidi ya Uzawa wa Mtume Muhammad {SAW} hapo Temeke Jijini Dar es salaam.


 Makamu wa Rais Mstaafu wa Tanzania Dr. Moh’d Gharib Bilal akitoa salamu kwenye  Maulidi ya Mtume Muhammad { SAW }yaliyoffanyika kwenye  Msikiti wa Ijumaa wa Majmuati Islamia Temeke Mjini Dar es salaam.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza katika hafla ya Maulidi ya uzawa wa Mtume Muhammad {SAW } yaliyoandaliwa na Uongozi wa Msikiti wa Ijumaa wa Majmuati Islamia Temeke Mjini Dar es salaam.

Picha na – OMPR – ZNZ.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.