Habari za Punde

Kongamano la Asasi za Kirais Zanzibar Litakalofanyika Katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini na Kushirikisha Washiriki 150 Kutoka Asasi za Kiraia..

Mkurugenzi wa Mradi wa Kusaidia Watendaji Wasio wa Kitaifa wa Zanzibar Frangois Dronnet, akizungumza na Waandishi wa habari wa Vyombo mbalimbali vya habari vilioko Zanzibar katika ukumbi wa hoteli ya Mazsons shangani kuhusiana na Kongamano la Asasi za Kiraia Zanzibar litakalofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Beach Resort mazizini Zanzibar na kuwakutanisha Watendaji 150 wa Asasi hizo.
Amesema imebainika baada ya utafiti uliofanywa kuna Asasi nyingi hapa Zanzibar zinakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo za kitaaluma,kukosa utaalamu  wa  kutosha wa kiuongozi na mambo ya utawala pia kuratibu masuala yanayohusu fedha.
Kongamano hili la siku mbili linadhaminiwa na Jumuiya ya Ulaya chini ya Mradi wa Kusaidia Watendaji wa Asasi za Kiraia (Non-State ActorsSupport Programme -ZANSASP, Mradi wa miaka mitatu unaotekelezwa kwa pamoja baina ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya uangalizi Wizara ya Fedha Zanzibar na ZANSASP.
Mkurugenzi wa Kusaidia Watendaji Wasio wa Kitaifa wa Zanzibar Frangois Dronnet akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari madhumuni ya Kongamano hilo la Asasi za Kirais Zanzibar litakalofanyika kuaazia tarehe 25-26-1-2017 katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar na kutowa elimu kwa Viongozi wa Asasi mbalimbali za Kirais za Unguja na Pemba juu ya kuongoza asasi hizo.
Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo wa kutowa taarifa ya madhumuni ya Kongamano hilo la Asasi za Kirais Zanzibar mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Mazson shangani Zanzibar na kuwashirikisha waandishi wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar,
Mjumbe wa Mradi huo kutoka Milele Bi KhadijaSharif akizungumza wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari kuhusiana na lengo la Kongamano hilo la Asasi za Kirais Zanzibar.
Mjumbe kutoka Taasisi ya TAYI Abdallah Ahmed, Suleiman akizungumza na waandishi wa habari faida itakayopatikana na Kongamano hilo kwa Viongozi wa Asasi za Kiraia Zanzibar katika kuongoza Taasisi zao katika njia ya mafanikio zaidi kwa jamii.
Afisa Uhusiano wa ZANSASP Ali Sultani akitowa ufafanuzi kwa waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakati wa mkutano huo wa kutowa malengo ya Kongamano hilo la Asasi za Kiraia Zanzibar linalotarajiwa kuaza kesho 25-na 26 katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Beach Resort mazizini Zanzibare na kuwashirikisha Viongozi 150 kutoka Asasi hizo za Kiraia Unguja na Pemba.
Waandishi wakifuatilia mkutano huo.
Mjumbe Kamati ya Maandalizi ya Kongamano hilo Bi Munira Homuod akitowa maelezo kwa waandishi wa habari na kujibu maswali yalioulizwa wakati wa mkutano huo na waandishi uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya mazson shangani zanzibar.



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.