Na Salmin Juma, Pemba
Wanajumuia ya “HAKI JAMII” inayojishuhulisha na kupinga matendo ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia nchini iliyopo Wilaya ya Chake Chake wamesema kua wameamua kujipanga vyema kupambana na matendo hayo na kero mbalimbali zinazo zinazoikabili jamii ili kufanikisha makundi yanayonyanyaswa kuishi kwa furaha kama ilivyo kwa watu wengine.
Hayo yameelezwa na Msaidizi Mwenyekiti Bw Kombo Ali Khamis wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa Habari huko Ofsini kwake Chanjamjawiri mkoa wa kusini pemba ambapo amesema vitendo vya udhalilishaji ni janga kubwa kwa taifa na kadiri ya siku zinavyosonga ndivyo vitendo hivyo vinaongezeka.
Akizungumzia katika mikakati waliyoipanga ili kukomesha matendo hayo amesema kua, kitu cha kwanza watazidisha kasi ya utoaji elimu kwa jamii juu ya madhara yatokanayo na matendo hayo.
“tumeanzia katika skuli mbalimbali, pia tunampango wa kuelekea kwa viongozi wa shehia kisha wanajamii wenyewe,tunaimani kua kasi hii itapunguza kiwango kikubwa cha matendo haya’ alisema Khamis.
Katika hatua nyengine M/kitu huyo amefahamisha kua, wameshaanza hatua madhubuti za kupambana na utumiaji wa madawa ya kulevya unaosababisha kuongezeka kwa matendo maovu yanayo fanywa na vijana wanaotumia madawa .
Amesema elimu ndio kitu cha msingi kwao,hivyo pia wameshaanza kuwatafuta watumiaji wa madawa hayo na kuwapatia elimu hukUwakiwaonyesha kiundani kabisa madhara yatakayoendelea kujitokeza iwapo kama hawatoachana na hali hiyo.
Mwisho kabisa ametoa wito kwa Serikali na mashirika binafsi na kila mdau wa hayo kushirikana kwa pamoja kupiga na kutokomeza matendo machafu ya udhalilishaji kwani jamii inaendelea kuteseka na janga hilo.
No comments:
Post a Comment