Habari za Punde

Unakumbuka mkate wa Boflo ulipokuwa Dili?

Mojawapo ya Bekari ya mikate ya miaka ilee 

(Picha kutoka maktaba ya Narendra Gajjar)

Picha hii inanikumbusha miaka ilee ambayo ulikuwa ukiutaka mkate lazima ukapange foleni bekari unaweka jiwe kwanza mapema kama alama ya foleni yako halafu ukija unalikuta limeshawekwa nyuma wakati ulikuwa wa mwanzo!. 

Unaweza kukaa masaa kadhaa kwenye foleni ukisubiri mkate na inapoanzwa kuuzwa mara kibiru kila mmoja anagombania. Halafu unarudi nyumbani na mkate uliotumwa hukuupata na familia inakusubiri wewe! 

Acha kumbukumbu ibaki kumbukumbu!

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.