Na.Aron Msigwa –NEC. 25/1/2017.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeeleza kuwa Kura 234 ziliharibika katika Uchaguzi mdogo wa Ubunge katika jimbo
la Dimani, Zanzibar Januari 22, 2017.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw.
Ramadhan Kailima amesema kuwa Wapiga Kura walioandikishwa katika jimbo la Dimani,
Zanzibar ni 9,275.
Amesema kati ya hao wapiga Kura 6,406 walijitokeza kupiga
Kura siku hiyo ambapo Kura halali zilikuwa 6,172 na Kura zilizoharibika zilikuwa
234.
“Napenda kuwafahamisha wananchi wote kuwa taarifa sahihi za matokeo ya
Kura katika Uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Dimani ni kama ifuatavyo; Wapiga Kura
walioandikishwa jimbo la Dimani ni 9,275, Waliopiga Kura walikuwa 6,406, Kura
halali 6,172 na Kura zilizoharibika ni 234” Amesisitiza.
Mkurugenzi Kailima ameeleza kuwa katika Uchaguzi huo vyama 11
vilikuwa na wagombea wa Ubunge ambapo Chama cha ACT-Wazalendo kilipata Kura 8, Chama
cha ADC Kura 42, Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kura 4860, CHAUMA Kura 10, Chama Cha
Wananchi CUF Kura 1234, Chama cha DP Kura 8.
Vingine ni Chama cha NRA kura 1, SAU Kura 4, TLP kura
2, Chama Cha UMD Kura 2 na Chama Cha UPDP Kura 1 na kufanya jumla ya Kura
za Vyama vyote kuwa 6172.
No comments:
Post a Comment