Na Salmin Juma, Pemba
Wananchi wa Gombe na Nguuni Shehia ya Shumba Vyamboni wameshauriwa kuitumia fursa waliyoipata kwa kuunga huduma ya maji safi na salama katika majumba yao .
Ushauri huo umetolewa na Afisa Mdhamini Wizara ya Ardhi Maji Nishati na Mazingira Juma Bakar Alawi wakati alipokwa akikabidhi mipira ya maji ZAWA kwa wananchi wa shehia hiyo kwa mashirikiano ya Mamlaka ya maji na Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni .
Amesema wameweza kuwafikishia wananchi huduma hiyo ya maji safi na salama ili kuwaondolea kero ambayo iliokuwa ikiwasumbua kwa muda mrefu na kuwataka kuichangia huduma hiyo.
Nae Mkurugenzi wa ZAWA Omar Bakar Mshindo amesema kuwa ufungaji wa mita kwa wananchi wanaohitaji kuungiwa huduma ya maji ni jambo la lazima kwani fedha zinazochangiwa na wananchi zinatumika kwa ajili ya manunuzi ya baadhi ya vifaa .
kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni Hamad Mbwana amesema upatikanaji wa mipira hiyo ya kusambazia huduma ya maji kwa wananchi ni kupitia fedha za mfuko wa Jimbo ambapo jumla ya maroli saba yenye thamani ya sh million saba yamenunuliwa .
Baadhi ya wananchi wa shehia hizo wameishukuru serekali ya mapinduzi ya zanzibar kupitia wizara ya Ardhi maji na Nishati kwa juhudi kubwa iliochukua ya kuwapelekea huduma ya maji safi na salama katika vijiji vyao.
No comments:
Post a Comment